TANGAZA NASI

header ads

Viongozi mbalimbali wawasili Chad kushiriki mazishi ya Deby



 Viongozi mbalimbali wa kigeni wameendelea kuwasili nchini Chad kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Idriss Deby wakati Ufaransa ikiunga mkono viongozi wapya wa kijeshi katikati mwa kitisho cha waasi cha kufanya mashambulizi katika mji mkuu wa N'Djamena. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, rais wa Guinea Alpha Conde na wakuu kadhaa wa nchi za kiafrika waliwasili mjini N'Djamena licha ya waasi kuwaonya viongozi wa kigeni kutohudhuria mazishi ya Debby yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa kwasababu za kiusalama. 

Baraza la kijeshi linaloongozwa na Jenerali Mahamat Idriss Deby mwenye umri wa miaka 37, lilichukua madaraka baada ya kifo cha baba yake ambaye ametawala kwa miaka 30 na alikuwa mshirika wa karibu wa mataifa ya magharibi.

Post a Comment

0 Comments