TANGAZA NASI

header ads

Ujerumani kutoa chanjo ya corona kwa wananchi wote kufikia mwezi Juni

 



Ujerumani inatarajiwa kuwapatia chanjo ya virusi va corona wakaazi wake wote ambao wako tayari kuchanjwa kufikia mwezi Juni. 

Waziri wa afya Jens Spahn ametoa makadirio hayo katika baraza la juu la bunge la Ujerumani, akiongeza kuwa hadi sasa karibu asilimia 21.6 ya idadi ya wakaazi wa Ujerumani tayari wamepatiwa dozi ya kwanza. 

Wakati huohuo rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier jana, alisaini marekebisho ya sheria ambayo ilipitishwa na baraza la juu la bunge la Ujerumani, na kuipatia serikali ya shirikisho mamlaka zaidi ya kuanzisha vizuizi vya nchi nzima vya kukabiliana na Covid-19. 

Miongoni mwa hatua zinazoweza kuchukuliwa ni marufuku ya nchi nzima ya kutotoka nje usiku katika maeneo ambayo yana na idadi kubwa ya maambukizi pamoja na shule kufungwa.

Post a Comment

0 Comments