TANGAZA NASI

header ads

Biashara 148 zafungwa kwa kipindi cha miezi 3 mkoani Njombe,madeni yatajwa kuchangia

 




Na Amiri Kilagalila,Njombe


Jumla ya biashara 148 zimefungwa kwa kipindi cha kuanzia January 1,2020 mpaka March 31,2021 mkoani Njombe  kutokana na sababu mba mbali pamoja na madeni  kwa wafanyabiashara yakichangia huku biashara 486 zikifunguliwa kwa kipindi hicho.


Hayo yamebainishwa na meneja msaidizi wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Njombe upande wa ukaguzi ndugu George Mapunda,wakati wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika mkoani hapa.



“Shida kubwa iliyopo wanasema kwamba mtu anakadiliwa kodi kubwa ambayo sio sahihi ila tatizo naona lipo kwenye utunzaji wa kumbu kumbu na sisi tunawatoza wafanyabiashara kutona na mauzo”alisema George Mapunda


Aidha amesema mkakati wa mamlaka hiyo kwa sasa ni kupita mlango kwa mlango ili kuzidi kutoa elimu zaidi juu biashara na ulipaji wa kodi huku akikili pia elimu hiyo inaendelea kutolewa mkoani Njombe


“Mkakati wetu ni kupita mlango kwa mlango kwasababu kuna mtu anaweza akakuandikia barua amefunga biashara lakini inawezekana hajafunga,na mwingine pia unakuta ana nia ya kufunga ila tukamuelimisha  na akatengua maamuzi yake”alisema  George Mapunda



Aliongeza kuwa “Kuna mwingine anapokutana na vikwazo ukamuelimisha na kumuelekeza kitu cha kufanya kama una deni njoo tukae kwasababu deni halimsababishi mtu afunge biashara.Kama unadaiwa na mamlaka utakuja tutajenga utaratibu wa kulipa kwa awamu”alisema Mapunda


Vile vile amesema kazi ya mamlaka hiyo sio kufunga biashara ya mtu “Mamlaka ya mapato haifungi biashara ya mtu,kuna watu wanadaiwa lakini hatufungi biashara ya mtu,tunachotaka tunakuita tunakaa mezani tunakwambia ulipe na deni lako ni hili kasha tunaingia kwenye makubaliano na mtu analipa kwa awamu”alisema George Mapunda



Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ametoa wito kwa wataalamu kutafuta jawabi la kina juu ya baishara kufungwa kwa kuwa haina afya kwa jamii.


“Kama hatuumii kuona watu 148 wanaacha biashara kwasababu tumepata 486 tutakuwa tuna mapungufu ninaomba tulitafakari kwa kina kwanini mtu anaamua kuacha biashara bila ya mtu kubadili na sio kuacha kwasababu biashara ni maisha yake na ni chaguo lake”Alisema Ruth Msafiri



Msafiri ametoa wito kutofurahia uwingi wa ukusanyaji mapato badala yake kutafakari juu ya wachache waliofunga biashara.


“Tusifurahie uwingi wa pesa tunazopata kwasababu tumekwenda kukusanya mpaka ziada lakini kuna watu nyumbani wanalia maisha hayaendi,ni vema tuangalie kila mmoja kwanini Yule ameacha biashara imekuaje?”alisema Ruth Msafiri


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Lubirya,ametoa wito kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuzingatia zoezi la utoaji wa elimu ili kufikia malengo chanya ya ukusanyaji mapato.



“Mkikumbuka maneno ya Mh! Rais ambayo amewaasa kuhusu mamlaka ya mapato watende kama inavyotakiwa ni ujumbe mzito ambao tukiuzingatia hakika utaonyesa mafanikio lakini pia tuzingatie swala la utoaji wa elimu”alisema Marwa Lubirya

Post a Comment

0 Comments