TANGAZA NASI

header ads

Wahalifu, walawiti watumia mtindo wa kuwalaghai kushiriki unyanyasaji wa kingono



 Wahalifu na walawiti wa watoto wanajaribu kuwalaghai na kuwatumia vibaya watoto ndugu watoto kama sehemu ya unyanyasaji wa kingono unaoibukia na kusambaa kwenye intaneti duniani, wataalamu wanasema.

Shirika linalofuatilia uhalifu wa aina hiyo kwenye mtandao - Internet Watch Foundation(IWF) limesema kuwa waathiriwa ni watoto wavulana wenye umri wa kati ya miaka 3 na 16, huku baadhi wakiandaliwa kunakili ponografia ya watu wazima.

Wakfu huo ulibaini mifano 511 ya watoto nduguwaliojaribiwa kuingizwa kwenye mtandao huo baina ya miezi ya Septemba na Disemba.

Karibu tukio moja kati ya matukio 30 yote "ya maudhui yalitengenezwa binafsi " katika wakati ule.

Wanaharakati wa matangazo ya moja kwa moja ya mtandaoni (livestreaming )wanasema huduma hiyo inahitaji kufanya juhudi zaidi katika kuwalinda watoto.

IWF, ambao inafanya kazi kwa ushirikiano na polisi na mitandao mbali mbali, inasema janga la Covid-19 lilipunguza maudhui yenye madhara" kwa unyanyasaji.

Mara nyingi tukio hilo huanza kwenye majukwaa yamitandao yakijamii na michezo(game) ya intaneti, kabla ya wahalifu hao kuwashawishi watoto kujiunga na huduma ya mazungumzo kwa njia ya video au ya matangazo ya moja kwa moja, ambako unanyasaji unaanza kufanyika

Unyanyasaji huu ulikuwa ni kitu kilichozoeleka katika nchi masikini zaidi awali miongoni mwa nchi masikini- lakini video ya IWF inaonesha pia watoto kutoka mataifa ya magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza na mataifa ya Ulaya wakinyanyaswa.

Jinsi magenge haramu yanayowauza wanawake kingono na kuwalazimisha kuwa makahaba Scotland

Post a Comment

0 Comments