TANGAZA NASI

header ads

Wazazi washauriwa kuwafikisha mapema watoto wanaoishi na VVU katika vituo vya afya

 


Joyce Joliga,Songea

Wazazi wenye watoto wenye ulemavu ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi  mkoani Ruvuma wameshauriwa kuwapeleka kupata matibabu  ikiwemo dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ARV ilikuwaepusha na magonjwa nyemelezi.

Mganga mfawidhi Hospitali ya mkoa wa Ruvuma  Dkt.Magafu Majura amesema,ni haki ya kila mtu kuishi,hivyo makundi hayo maalumu ya watoto wenyeulemavu hayapaswi kufichwa na kufungiwa ndani  kwa sababu ya ulemavu au      ugonjwa wa ukimwikwani nao wana haki ya kuishi na kupata mtibabu kama Binadamu yoyote.

“Jamii iache tabia ya kuwafungia ndandi watoto wenye ulemavu ambao wanaishi na virusi vya ukimwi ,huo niunyanyapaa bali wawasaidie kuwapeleka kwenye kliniki (CTC) ili wapate ushauri na  matibabu ,kwani kupata huo ugonjwa siyo mwisho wa maisha bali ni mapenzi ya Mungu hivyo wawapende na kuwapatia lishe nzuri , ili kuwajengea kinga”,alisema Dkt.Majura.

Amesema,kasi ya ongezeko la maambukizi mapya ya ukimwi yamepungua mkoani Ruvuma kutokana na wananchi kuchukua tahadhali  na kuacha kufanya ngono zembe

Naye Magdalena Bikulema amewataka wazazi wanaoishi na watoto wenye ugonjwa wa ukimwi kuachana na imani potofu kuwa watoto wao wamerogwa na kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji  kwani vitendo hivyo vinachangia vifo vya watoto wenyeulemavu.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma  Brigedia Jenerali ,Balozi Wilbert Ibuge alisema, Mkoa wa Ruvuma umeendelea na mapambano dhidi ya ukimwi ambapo hadi kufikia mwezi Oktoba, 2021, maambukizi ya Ukimwi yamepungua hadi kufikia 5.6% kutoka 7% mwaka 2015, hivyo maambukizi ya Ukimwi toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto yamepungua hadi kufikia 4%.


Post a Comment

0 Comments