Njombe
George Lupindu (19) mkazi wa kijiji cha Ngalawale wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,amehukumiwa na mahakama ya wilaya mkoani hapo kutumikia kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9.
Akisomewa hukumu hiyo na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 37/2021 George Lupindu ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(3) cha Kanuni ya Adhabu, Sura namba 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa Mapitio mwaka 2019.
Imeelezwa na Mwendesha Mashtaka Asifiwe Asigile kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai 7 mwaka huu ambapo anadaiwa kumrubuni mtoto huyo (jina limehifadhiwa) wakati akitokea shuleni kwa kumdanganya kuwa anampeleka nyumbani kwao na kisha kumkamata kwa nguvu na kutenda kosa hilo.
0 Comments