TANGAZA NASI

header ads

Ludewa:Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka Bibi

 



Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mahakama ya wilaya ya Ludewa iliyopo  mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elias Mgaya (20) mkazi wa kijiji cha Madilu wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kosa la kumbaka bibi kizee wa miaka 70.


Akisomewa hukumu hiyo na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 32 la mwaka 2021 Elias Mgaya ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130 (1) (2)(c)na 131(1) Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2019.


Awali akisomewa sitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asigile imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo machi 29  mwaka huu ambapo alimvamia bibi huyo(jina lake limehifadhiwa) nyakati za usiku akiwa amelala na kisha kutenda kosa hilo.

Post a Comment

0 Comments