TANGAZA NASI

header ads

Mawaziri 2020-2025 waapishwa

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri 21 na manaibu waziri 23 aliowateua ilikukamilisha baraza la mawaziri

Uapisho huo umefanyika leo, jijini Dodoma, katika Ikulu za Rais, Chamwino mara baada ya uteuzi wake Desemba 5,2020, Mawaziri walioapishwa leo wana kwenda kuunda baraza la mawaziri la Tanzania.

Walioapishwa kuwa mawaziri ni pamoja na William Lukuvi- wizara ya Ardhi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Innocent Bashungwa, Wizara ya Afya- Dk Dorothy Gwajima, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa- Elias Kwandikwa, Utumishi na Utawala Bora- Kapten John Mkuchika, Wizara ya Maji- Juma Aweso, Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu- Jenista Mhagama,Ofisi ya Rais Uwekezaji- Profesa Kitila Mkumbo.

Pia Dk Mwigulu Nchemba, Wizara ya Elimu- Profesa Joyce Ndalichako,Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Mashimba Ndaki, Wizara ya Maliasili na Utalii- Dk Damas Ndumbaro, Tamisemi- Suleiman Jafo, Wizara ya Nishati- Dk Medard Kalemani,Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Dk Leonard Chamuriho, Wizara ya Kilimo- Profesa Adolf Mkenda,Wizara ya Madini- Doto Biteko,Wizara ya Viwanda na Biashara- Godfrey Mwambe, Wizara ya Mambo ya Ndani- George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Ummy Mwalimu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Dk Faustine Ndugulile.

Aidha walioapishwa kuwa manaibu waziri ni; Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka, Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi, Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi, Wizara ya Fedha- Mwanaida Ali Khamis, Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar, Tamisemi- Dk Festo Ndugange, Wizara ya Nishati- Stephen Byabato, Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Kundo Mathew, Wizara ya Mifugo- Pauline Gekul.

Wengineo ni Wizara ya Madini- Ndulane Kumba, Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya, Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga, Wizara ya Maji- Maryprisca Mahundi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Abdallah Ulega, Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Mwita Waitara, Wizara ya Mambo ya Nje- William Olenasha,Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja, Ofisi ya rais Tamisemi- David Silinde, Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe, Wizara ya Afya- Dk Godwin Mollel, Wizara ya Katiba na Sheria- Pinda Mizengo.

Post a Comment

0 Comments