Na
Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri
Kanoni ameelekeza viongozi wa wilaya hiyo na kata ya Igima Kuhakikisha wanasimamia
kikamilifu ukusanyaji wa Michango ya ujenzi wa bweni Jipya la wavulana katika
Shule ya sekondari Igima lililoungua Moto Mwezi Septemba mwaka huu na kuteketeza
Kila Kilichokuwamo Ndani pasina Kuleta Madhara Kwa Wanafunzi Wenyewe.
Ametoa agizo hilo wakati akipokea mifuko 250 ya
Saruji Toka Shirika la Nyumba La Taifa NHC Kwa ajili ya Kuanza Ujenzi wa Bweni
Hilo na Kwamba Makubaliano ya Mchango wa Shilingi Elfu Kumi Kila Mwananchi
Yatekelezwe Haraka Kabla Hatua za Kisheria Hazijaanzachukuliwa.
“Naelekeza mtendaji wa kijiji,kata na bodi ya shule
vile viwango ambavyo kila mwananchi inatakiwa achangie lazima achangie basi
achangie na ikipendeza kabla ya tarehe 25 jengo liwe limesimama na vimebakia
vitu vidogo vidogo”alisema Lauteri Kanoni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe
Edec Lukoa amesema kutokana na changamoto ya kupanda kwa saruji Katika kipindi
kilichopita kiliwalazimu kusimamisha ujenzi wa bweni Hilo Lakini Kwa Wanaendelea na Hadi kukamilika linatarajiwa
kutumia zaidi ya Shilingi Milioni 75 fedha ambazo Ni michango ya
Serikali,Wananchi Pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo.
“Hilo bweni liliungua lote kabisa na watoto kama 90
walitoka salama wenzetu shirika la nyumba walipokea ombi letu na waliahidi
kutusaidia kama tulivyoomba”alisema
Lukoa
Said Bungara Ni Meneja wa Shirika la Nyumba NHC
mikoa ya Njombe,Iringa na Mbeya ambaye anasema wao Kama Wadau baada ya kupewa
taarifa ya kuungua kwa Bweni Hilo waliona Ni muhimu kuchangia Nusu ya mifuko ya
saruji ili wanafunzi waendelee kuishi
Katika mazingira salama.
“Shirika la nyumba ni wadau wa maendeleo na tunaunga
mkono jitihada za serikali yetu na tuliposkia kuna jambo la kuchangia kwa
watoto wetu tukasema na sisi tujitoe vile ambavyo tunaweza na tukatoka mifuko
250 ambayo ni sawa na tani 12.5”alisema Said Bungara
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igima Mika
Mbembati na Judy Kinyamagoha Wamesema Hatua Zinazoendelea Kuchukuliwa na
Serikali Katika Ujenzi wa Bweni Hilo Zinawapa Matumaini ya Usalama wa Maisha
Yao Pamoja na Masomo Huku mkuu wa shule hiyo Edwin Sanga Akishukuru kwa msaada
huo na kuwaomba Wadau mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono Kwa Kuwa Bado Kuna
Uhitaji Mkubwa wa Mabweni.
0 Comments