Serikali imesisitiza kuendelea kurejesha mali zote za vyama vya ushirika, zilizochukuliwa kwa hila na wizi, ambapo hadi sasa mali 59 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 68 na milioni 900 zimerejeshwa kwenye vyama hivyo.
Msisitizo huo wa serikali, umetolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya, wakati alipokuwa akifungua kongamano la uwekezaji wa Benki ya Kilimanjaro Co-operative Bank Limited (KCBL).
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira, ambaye ndiye aliyefanya juhudi za kuhakikisha benki ya (KCBL) inafufuka, ameweka bayana malengo na ndoto walizonazo kuwa na benki ya taifa ya ushirika.
Nao wawekezaji wa benki ya (KCBL), benki ya CRDB na Kilimanjaro Development Forum (KDF), wakawataka wanaushirika kuikimbilia benki hiyo kwa kununua hisa, kwani ushirika ndio silaha kubwa kwenye maendeleo.
0 Comments