TANGAZA NASI

header ads

Njombe:Walia na unyanyasaji wa kijinsia "Ninapigwa na mke wangu"



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Ukatili wa kijinsia na ukatili wa kingono mkoani Njombe umetajwa kuwa chanzo kikubwa cha kurudisha nyuma  maendeleo ya wanchi hususani vijijini kutokana na ukosefu wa elimu kwa wananchi na kutambua haki zao.

Wananchi wa kijji cha Utengule kata ya kifanya wanalia na changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia  katika maeneo yao  tatizo  ambalo limeibuliwa na UN WOMEN shirika linalo  jihusisha na ulinzi wa mama na mtoto pamoja na kupinga udhalilishaji dhidi ya wanamke na watoto .



“Mwanamke anatoka kujifungu hata wiki tatu hajamaliza,mwanume anaanza kumpalamia yaani mpaka mwingene anahama chumba kwenda kulala kwa watoto lakini bado mwanaume anang’ang’ania nataka unataka nini kwanini usimvumilie”Teopista Mkongwa mkazi wa Utengule mjini Njombe

Blasio Mkongwa naye amesema amekuwa akipigwa na mke wake

“Ninapigwa na mke wangu,nikiona kuna dalili za kupigwa wakati mwingine kuna baadhi ya vitu hatari ndani ya nyumba yangu inabidi nivichukue nivifiche.wanawake safari hii wamekuwa na nguvu kuliko sisi wanaume” Alisema Blasio Mkongwa



Licha ya UN WOMEN Kufika kijijini hapo kutoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono wananchi bado wanahitaji elimu ya afya ya  uzazi kwani tatizo la wanawake kulazimishwa kingono mara tuu baada ya kujifungua ni changamoto kwao.

Lucy Tesha anafanya kazi kitengo cha kutokomezea ukatili wa kijinsia kutoka ofisi ya umoja wa Mataifa UN unao shughulika na usawa wa kijinsia na uelimishaji wa wanawake anawasa wananchi kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi .



“Kuna wadada wanaopiga vizuri waume zao,wale wapigaji acheni haya matukio yanatokea lakini wanaume hawaripoti na wanafanya hivyo kwasababu ya kuogopa kudharauliwa na kuona ataonekana ni mwanaume gani,hii sio sawa” Lucy Tesha kutoka kitengo cha kutokomezea ukatili wa kijinsia ofisi ya umoja wa Mataifa UN

Daniel Mwasongwe Mratibu wa kidhibiti ukimwi halmashauri ya mji Njombe amekiri uwepo wa ukatili mjini Njombe na kusema kuwa kuanzia mwezi januari mpaka sasa kesi 25 za Watoto kuanyiana ukatiliwa kingono zimeripotiwa ,kesi 29 watu wazima wakiwafanyia akili wa kingono Watoto,watu 384 wametelekeza Watoto,watu 154 wamefanyiwa ukatili wa kimwili,watu 54 wamefanyiwa ukatili wa kiuchumi,watu 13 wamefanyiwa ukatili wa kihisi hii ikionyesha bado katika halmashauri yam ji Njombe ukatili bado umeendelea kushika kasi.

UN WOMEN shirika linalo  jihusisha na ulinzi wa mama na mtoto pamoja na kupinga udhalilishaji dhidi ya wanamke na watoto wanaendelea na zoezi la kutoa elimu dhidi ya jinsia ikiwa ni kampeni ya siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia na kulinda haki ya mwanamke na mtoto.


Post a Comment

0 Comments