Seneta Norma Durango amewasilisha muswada Bungeni nchini Argentina akipendekeza picha ya Legend wa soka Diego Maradona aliyefariki Novemba 25, iwekwe kwenye fedha za noti za Nchi hiyo (Peso 1,000 sawa na Sh 27,600.)
Durango amesema lengo ni kumuenzi nyota huyo kwa heshima aliyolipa taifa hilo mwaka 1986 baada ya kuwezesha Argentina kutwaa kombe la dunia.
Noti hiyo itaonyesha sura ya Maradona huku upande mwingine ikionyesha goli maarufu alilofunga kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Uingereza 1986.
0 Comments