TANGAZA NASI

header ads

Messi aweka rekodi mpya La Liga

 


Mshambuliaji na nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 25 kwenye ligi kuu nchini Hispania kwa misimu 12 mfululizo, mshambuliaji huyo amefikia rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Getafe.

Mabao mawili aliyofunga Messi yamemfanya afikishe mabao 25 msimu huu kwenye La Liga na ndio kinara wa ufungaji akiwa anaongoza kwa tofauti ya mabao 4 dhidi ya Karim Benzema wa Real Madrid mwenye mabao 21.

Post a Comment

0 Comments