Na Amiri Kilagalila,Njombe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea
wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt,John Pombe
Magufuli,ametuma salamu za pole pamoja na ubani wa shilingi milioni tano kwa
familia ya Mlelwa,kufuatia mauaji na kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa wanafunzi
wa vyuo na vyuo vikuu (UVCCM) mkoa wa Iringa Ndugu,Emmanuel Mlelwa
Akitoa salamu za pole katika mazishi yaliyofanyika
kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa,mkoani Njombe,katibu wa NEC
Uchumi na fedha wa Chama hicho ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Njombe
Dkt,Frank Hawasi.Amesema Rais Magufuli amesikitishwa na kifo cha kijana huyo
kutokana na umuhimu wake kwa familia na taifa.
“Mwenyekiti wetu amepokea taarifa ya kifo cha kijana
wetu Emmanuel Mlelwa kwa masikitiko makubwa sana,kwasababu sio kifo cha
kawaida,lakini pia umuhimu wa kijana mwenyewe kwa nchi kwa ujumla”Alisema Dkt,Hawasi
Amesema Rais Magufuli amelaani
kitendo hicho kwani hakikubaliki katika jamii“mwenyekiti wa CCM Taifa analaani
kitendo kilichofanyika kwa ndugu yetu Emmanuel Mlelwa kwasababu hakionyeshi
utu,hakionyesho uzalendo na hakionyeshi utanzania wetu”aliongeza Dkt. Frank
Hawasi
Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa kupitia kwa katibu wa
NEC Uchumi na Fedha wa Chama hicho taifa Dkt,Frank Hawasi.Ameagiza vyombo vya Dola
mkoani Njombe kuwatafuta na kuwabaini waliohusika na mauaji ya kijana huyo.
0 Comments