Na Prosper Mfugale,Ludewa
Asilimia za Ufaulu mitihani ya darasa la saba na la
nne katika shule za msingi 24 kutoka kata 6 wilayani ludewa mkoani Njombe
zimeanza kupanda Katika maeneo kunakotekelezwa mradi wa MAMMIE kupitia
shirika la maendeleo kusini mwa Tanzania SHIPO kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la we world ambapo shule
ya msingi mavala kutoka kata ya milo imefanikiwa kuchomoza na kuongoza katika
mtihani wa darasa la saba kwa shule zote za serikali wilayani humo.
Shule hizo zipo katika kata za milo, lubonde,mlangali,madope,mawengi,na
luana ambazo zimejengewa miundombinu ya majengo yakiwemo madarasa, ofisi
,majiko ,mabwalo ya chakula, matundu ya vyoo na miundombinu ya maji
Shirika la Shipo katika taarifa yake kupitia mratibu
wa mradi wa MAMMIE bwana nemes temba kwenye kilele cha madhimisho ya wiki ya elimu duniani
yaliyofanyika katika shule ya msingi mavala hapo may 5, 2021 alieleza kuwa juma la elimu duniani hufanyika kila mwaka
ifikapo apri 26-30 lakini mwaka huu siku
maadhimisho yamesogea mbele kutokana na kuingiliana na ratiba za mitihani za
wilaya ya ludewa
Aliongeza kuwa kauli mbiu ya juma la elimu kwa mwaka
2021 ni wezesha elimu stawisha jamii ambapo alisema siku hiyo ipo katika ajenda
17 zaa maendeleo endelevu kwenye lengo
namba nne linalosisitiza kutoa elimu ya usawa, elimu jumuishi
Tangu mwaka 2014 shirika la shipo baada ya kutambua
kuwa changamoto mbalimbali zilizopo katika shule za msingi hurudisha nyuma
jitihada za kupandisha ufaulu lilianza kubresha miundombinu katika shule hizo
kwa kusaidia ujenzi wa mindombinu kwa awamu ambapo mpaka sasa lipo katika awamu
ya tatu ndani ya kata hizo sita .
Licha ya kusaidia katika mradi huo shirika pia lilitoa mafunzo kwa walimu
wazazi na kamati za shule yanayohusu utawala bora ili kuwa na uelewa mpana juu
ya masuala yahusuyo elimu.
‘’hasa tuanasaidia katika kuboresha utawala na
usimamizi ,tunaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kama mujenzi wa
vyoo madarasa ,nyumba za walimu majiko na mabwalo ya chakula lakini pia
tunasaidia kuweka miundombinmu ya maji shuleni’’Nemesi temba mratibu mradi wa
mammie Shipo Njombe.
Shirika la Shipo pia lilitoa msaada wa miche ya miti
ya mbao na matunda ina ya parachichi katika shule za msingi 24 wilayani ludewa
kutoka kata 6 ili kusaidia kujiwezesha kiuchumi wakati wa kipindi cha mavuno.
‘’Kwa kata ya milo tulipokea miche 510 ya matunda
ambayo kwa sasa ina umri wa mika 3 na inatoa matunda na Watoto wanapata chakula
cha mchana huku wakifurahia mlo wenye matunda na mboga za majani. Alisema
sijali simindu afisa ogani kata ya milo
Kila mwaka shirika huadhimisha wiki ya elimu duniani ambapo siku hiyo shule
iliyofanya vizuri hupewa zawadi mbalimbali ikiwemo kombe la elimu Pamoja na
shughuli mbalimbali ambazo hufanyika kwa lengo la kuhamasisha wazazi kuona
umhimu wa elimu kwa Watoto wao na kuongeza ari ya masomo kwa wanafunzi kwa
kuwapa zawadi mbalimbali vikiwemo vifaa vya vya shule .
Mwaka huu 2021 kilele cha wiki ya elimu kimefanyika
katika katika shule ya msingi mavala kata ya milo shule ambayo pia ilifanya
vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2020 na kuibuka mshindi kwa shule
zilizopo katika mradi kwa kuwa nafasi ya kwanza ambayo ilijinyakulia zawadi
mbalimbali likiwemo kombe la elimu.
Shule hii pia iliongoza shule za serikali katika
mtihani huo wa mwaka 2020 kwa kushika nafasi ya kwaza na kuwa nafasi ya pili
kiwilaya baada ya kuongozwa na shule moja ya binafsi ikiwa ni matokeo chanya
yaliyotokana na mradi.
Kwa niaba ya wanafunzi wote wa shule ya msingi
mavala mwanafunzi judithi haule alitoa shukrani kwa shule hiyo kuchaguliwa
kuadhisha wiki ya elimu ambaye pia alilishukuru shirika kwa misada mbalimbali
linayoitoa ambayo imechangia taaluma kupanda.
Wageni mbalimbali walihudhuria katika siku hii mhimu
ya kilele cha wiki ya elimu akiwemo afisa elimu msingi wilaya ya ludewa Daniel
makorere ambaye alimwakilisha mkurugenzi ambaye Pamoja na mambo mengine
alilishukuru shirika la shipo Pamoja na wafadhili kwa kazi nzuri wanazofanya
katika idara ya elimu msingi huku akiwataka wazazi kuendelea kushirikiana nao.
Wazazi na walimu kutoka shule ya msingi mavala katika
siku ya maadhimisho wameleza namna walivyoshiriki katika kuinua elimu ikiwemo
ujenzi wa miundombinu na kushiriki katika mradi wa kilimo cha parachichi
ulioanzishwa shuleni hapo na wafadhili wa kutoka shirika la kimataifa la we
wold kupitia shirika la shipo kwenye
mradi wake wa mammie
Wa kwanza kulia pichani ni mwalimu mkuu wa shule ya
msingi Mavala wilayani Ludewa akikabidhiwa kombe la elimu na afisa elimu msingi
kutokana na shule hiyo kushinda kitaalamu kati ya shule zinazofadhiliwa na
mradi wa Mammie chini ya shirika la shipo
Baadhi ya walimu wakikabidhiwa
zawadi kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu yalifoanyika katika shule ya msingi
Mavala kata ya Milo
Baadhi ya walimu na watendaji wa shirika la Shipo
wakiwa katika picha ya pamoja
0 Comments