Aliyekuwa Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt,Faustine Ndungulile,Amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuhudumu katika serikali ya awamu ya tano mpaka nafasi yake ilipotenguliwa hapo jana.
Kupitia ukurasa wake wa Twita Ndungulile ameandika.
"Nimepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. Ninamshukuru sana JPM kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru sana @umwalimu na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia.
Mafanikio ya sekta ni makubwa sana. Namtakia kila la kheri NW ajaye Dkt Mollel" amesema Ndungulile.
Ndungulile ambaye ni mbunge wa jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi,amehudumu katika wizara hiyo takribani miaka mitatu tangu October 2017,alipoteuliwa na Rais Magufuli.
0 Comments