Na.Alex Sonna,Dodoma
MBUNGE wa Nanyamba(CCM), Abdallah
Chikota ameiomba serikali kusimamia upatikanaji wa magunia kwa wakati
ili kuzuia ubora wa korosho kutoathirika.
Sambamba na hilo, ameiomba Wizara
ya Kilimo kuhakikisha suala la upatikanaji wa vifungashio haliachiwi kwa
Bodi ya Korosho peke yake bali lihusishe hata vyama vya ushirika ili
kupunguza kabisa upungufu wa magunia katika msimu.
Akichangia leo Bajeti ya Wizara ya
Kilimo bungeni jijini Dodoma, Chikota amesema vifungashio vikipatikana
kwa wakati itasaidia kuhifadhi ubora wa korosho.
“Naiomba wizara isimamie ipasavyo
magunia yapatikane kwa wakati ili korosho zetu zisije kuathirika ubora
wake,lakini niiombe wizara pia siachie suala hili bodi ya korosho peke
yake bali vyama vya ushirika vihusike pia,”ameomba Chikota.
Ameshauri pia pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea ya sulphur zipatikane kwa wakati ili isiathiri msimu wa kilimo.
0 Comments