Rais John Magufuli amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imepungua sana, huku baadhi ya vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia wenye maambukizi vikiwa vitupu.
Rais amesema hilo wakati akitoa salamu kwa Watanzania alipohudhuria ibada ya Jumapili- KKKT Usharika wa Chato Mkoani Geita,
Akitoa takwimu hizo Rais Magufuli amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam;
Amana ilikuwa inalaza wagonjwa 198 leo walikuwepo watu 12 walioathirika, Mloganzila walikuwa watu 30 leo 6, Kibaha huwa wanalazwa watu zaidi ya 50 leo wamebaki watu 22 ambao hali zao ni nzuri.
Akitaja vituo vingine amesema Aga Khan wamebaki watu 31, Hindu Mandali wamebaki 16, Regency 17, TMJ wamebaki 7, Rabininsia wamebaki 14.
Katika mikoa mingine amesema, Arusha kuna vituo vitatu, Moshono kuna wagonjwa 11, Longido na Karatu hakuna mgonjwa.
Mwanza kuna vituo 10 ambapo Buswelu kuna wagonjwa 2, Misungwi 2 Ukerewe, Magu, Mkuyuni, Bachosa, Sengerema, Kwemba kote hakuna mgonjwa, huku Hospitali ya Bungando na Sékou Touré kuna wagonjwa 2 wenye uhitaji maalum.
Dodoma kuna vituo vinne ambapo mjini viko viwili kuna wagonjwa wawili huku Kongwa na Kondoa kukiwa hakuna hakuna mgonjwa.
“Mungu ametusaidia na kwa taarifa za leo wagonjwa wamepungua sana Amana ilikuwa inalaza Watu 198, leo walikuwepo Watu 12 tu, Mlogonzila ilikuwa inalaza Watu 30 leo wamebaki 6, pale Kibaha Hospitali ilikuwa inalaza zaidi ya Watu 50 leo wamebaki Watu 22” Rais @MagufuliJP
#JPMChato https://t.co/MGglzJQwzh
“Arusha moshono wamebaki 11, vituo vingine havina wagonjwa, Mwanza wana vituo kumi lakini wamebaki sita vituo vingine hakuna mgonjwa, Dodoma kuna vituo vinne kuna wagonjwa wawili walikuwa wagonjwa 42 wengine wote wamerudi nyumbani, Mungu amejibu maombi” Rais @MagufuliJP https://t.co/AQRxU1y696
“Mimi Mtoto wangu wa kumzaa amepata corona akajifungia, akajifukiza na kunywa malimao, sasa hivi ni mzima kabisa anapiga push-up, msije mkadhani mimi sijapata mtu wa karibu mwenye corona”- Rais Dtk. John Magufuli https://t.co/XAKYZx8DAh
0 Comments