TANGAZA NASI

header ads

RC MAKALLA AMALIZA MGOGORO WA MEYA NA MKURUGENZI KINONDONI



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza Kati ya meya manispaa ya kinondoni Ndg Songoro Mnyonge na mkurugenzi wa manispaa Spora Liana.


Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao Cha pamoja kilichoitishwa leo  na mkuu wa mkoa  na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni.


Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.


Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.



Post a Comment

0 Comments