TANGAZA NASI

header ads

Zanzibar yawakaribisha wawekezaji kutoka China



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano na Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China ulioasisiwa tangu mwaka 1964 baada ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.


Mhe. Heme alieleza hayo wakati akizungumza na Balozi mdogo wa China Bw.Zhang Zhisheng alifika afisini kwake Vuga kwa ajili ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo juu ya masula mbali mbali ya maendeleo baina ya pande mbili.


Akizungumzia sula la uwekezaji Makamu wa Pili wa Rais amemuhakikishia Balozi mdogo wa china Bw.Zhang Zhisheng kuwa serikali ya mapinduzi Zanzibar inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuekeza Zanzibar kwani mazingira yapo salama kwa ajili ya uwekezaji.

 

Nae Balozi Mdogo wa China Bw. Zhang Zhisheng amemuleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa China itaendelea kutoa mashirikiano yake kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na udugu wa kihistoria uliojengeka kwa muda mrefu sasa.


Bw. Zhang Zhisheng amesema China ni Taifa linalojali uhusiano na mataifa mbali mbali Afrika bila ya kujali utofauti wa ukubwa au udogo na mipaka ya kimaeneo, na kueleza kuwa China inaheshimu mambo ya ndani ya nchi ikiwemo masuala ya kisiasa.

Post a Comment

0 Comments