Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Shule za msingi na
sekondari halmashauri ya mji wa Makambako mkoni Njombe zinakabiliwa na uhaba wa
madawati 416 kwa shule za msingi na 834 kwa shule za sekondari ikiwemo viti na
meza kwaajili ya matumizi ya wanafunzi hali inayopelekea changamoto katika
utoaji elimu.
Hayo yamebainishwa katika
kikao cha baraza la madiwani na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Hanana Mfikwa pamoja
na mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo Paul Malala.Wamesema sio madawati bali
pia kuna uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo wamewaomba madiwani kuwahasisha
wananchi na wadau wengine kujitokeza kuchangia.
“Tuhamasishe wananchi
kuhakikisha wanachangia na kuondoa hili tatizo la madawati na meza kwa shule za
msingi na sekondari”alisema Malala
Naye hanana Mfikwa
alisema “Ni kweli watoto wamekuwa wengi na wanahitaji kupata huduma kwa hiyo
sambamba na hayo tukahamasishe ujenzi wa madarasa kwasababu miundombinu
haitoshi pia”alisema Hanana Mfikwa
Madiwani wa
halmashauri hiyo mara baada ya kupokea taarifa ya kushirikisha wazazi na wadau
uchangiaji wameshauri serikali kuwe na utaratibu wa uchangiaji vifaa kwa
wanafunzi wanaotoka katika shule za nje ya kata husika.
“Madawati haya ili
tuweze kufanikisha inabidi tufanye kama wilaya nyingine kwasababu unapopoeleka
kwenye wilaya nyingine wanasema itabidi utoa mchango wa madawati na huko
tunalipa shilingi elfu arobaini”alisema Edo
chaula diwani kata ya mwembe togwa
Aidha katika kikao
hicho madiwani wameonyesha kusikitishwa na kasi ya ukarabati wa barabara za
mijini na vijijini zinazosimamiwa na Tarura kwa kuwa maeneo mengi
yamekuwa na changamoto huku TARURA wakisema zinaendelea kukarabatiwa.
0 Comments