TANGAZA NASI

header ads

Serikali ya Zanzibar na Sektarieti ya Kitaifa imejipanga kumaliza changamoto za muungano

 



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarijika kwa mafanikio ya vikao vya Sektarieti ya Kitaifa ya kujadili hoja na Changmoto za Muungano, ambapo  jumla ya changamoto nane zinatarajiwa kutatuliwa katika kipindi kifupi kijacho.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Sektarieti ya Kitaifa inayojadili changamoto za Muungano, iliofika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Mheshimiwa Hemed, amesema mashirikiano mazuri  yaliyopo baina ya Ofisi yake pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais ni kutokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, aliyowapa watendaji wakuu chini ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunano wa Tanzania Mheshimiwa Philip Isdor Mpango.

Mapema Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungno na Mazingira Bi Merry N. Maganga pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tixon T. Mzonda kwa pamoja wamemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Sekretariti hiyo ipo inaendelea na vikao vyake ikiwa ni muendelezo wa kujadili na kuzipatia ufumbuzi hoja na changamoto zilizomo ndani ya Muungano.

Post a Comment

0 Comments