TANGAZA NASI

header ads

Njombe:Mwenyekiti mpya Njorefa aanza kwa kishindo,asiyeendana na kasi atakiwa kujiuzulu

 





Na Amiri Kilagalila,Njombe


Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Njombe hapo jana Thobias Lingalangala ameahidi kuanza mara moja ujenzi wa ofisi za chama cha soka mkoa wa Njombe (Njorefa).


Ahadi hiyo ameitoa baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo kwa kupata kura 18 na kumshinda mpinzani wake Yono Kevela aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho ambaye alipata kura 0.


Alisema yeye siyo mtu wa hadithi kwa kuwa hakuumbwa hivyo na kuahidi kuwa mtekelezaji wa mambo na kumtaka katibu wake pia kuwa mtu wa vitendo vinginevyo ajiuzulu mapema.


"Nataka ofisi ya Njorefa ijengwe mara moja hii nimeagiza ifanyije tathmini leo ili kesho nipewe ripoti na kesho kutwa ujenzi uanze" alisema Lingalangala.


Alisema kupata kura asilimia mia moja kutoka kwa wajumbe kwake ni deni kubwa hivyo.licha ya uhenzi wa ofisi hiyo ana mpango wa kwenda kuvumbua vipaji na kuvitambua vilabu vyote vya mkoa ili kuviwekea mazingira mazuri ya ushiri katika ligi.


Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Deogratiasi Mbisi alisema Lingalangala amechaguliwa kwa kura zote za wajumbe walioshiriki uchaguzi huo wapatao 18 pamoja na makamu wake Emmanuel Mbogela.


Pia alimtangaza Obed Mwakasungula kuwa katibu mkuu ambaye pia alipata kura 18 huku mpinzani wake Abubakar Aziz  ambaye hakuwepo kwenye uchaguzi huo akipata kura sifuri.


Kwa upande wa mwakilishi wa mkutano mkuu wagombea walikuwa watano ambapo Evans Nyinge aliibuka kidedea kwa kupata jumla ya kura 11 na kuwabwaga wapinzani wake.


Aidha Mbisi alimtangaza Lusubilo Mwakafuje kuwa mshindi katika nafasi ya kuwa mwakilishi wa vilabu.


Mara baada ya kupatikana kwa uongozi huo wapenzi wa soka mkoani Njombe  akiwemo Solanus Mhagama na Judith Sanga waliishukuru kamati ya uchaguzi pamoja na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kusimamia uchaguzi huo kwa uliofuata taaratibu zote.


" Tunamshukuru mungu kwani TFF kwa kushirikiana na kamati ya uchaguzi pamoja na uongozi wa serikali kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufuata utaratibu uliowekwa" alisema Solanus.


Hata hivyo Siku moja baada ya uchaguzi wa njorefa kufanyika ,kamati tendaji ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Thobias Lingalangala imeunda kamati mbalimbali ambazo zitasimamia maendeleo ya mpira mkoan humo na kutoa onyo kwa ataezembea na kuonekana kikwazo katika jitihada za kukuza soka


Akitoa ufafanuzi wa kuharakisha uundwaji wa kamati na Aina ya Viongozi wasiotakiwa katika kipindi hiki Cha kunusuru soka la Njombe ambalo linazidi kudidimia. Lingalangala Amesema yeyote atakaeonesha kushindwa kuendana na Kasi yake ajiengue kabla hajaenguliwa na Kisha kutoa agizo la uwajibikaji.


Kuhusu kamati zilizoundwa na wajumbe wake, makamu mwenyekiti wa njorefa amesema zipo 5 na kuwataja wajumbe wake pamoja Viongozi wa kamati hiyo ambao papo hapo wameingia kazini.


Kamati ambazo zimeundwa ni ni Kamati ya fedha ambayo mwenyekiti wake ni Erasto Mpete ,Kamati ya Ligi na Mashindano ambaye mwenyekiti wake Lusubilo Mwakafuje,Kamati ya Ufundi mwenyekiti akiwa ni Meshack Mnyawasa ,Huku Kamati Vifaa mwenyekiti wake akiwa ni Musa Muhagama 

Kamati zimeanza utekelezaji wa maagizo ikiwemo kuvitambua Tena vilabu vya ngaz zote vya mkoa wa Njombe,maandalizi ya ujenzi w ofisi na kuirejeshea makali Tena njombe mji ili kurejea kigi kuu misimu ijayo.


Post a Comment

0 Comments