TANGAZA NASI

header ads

MFANYABIASHARA TARIME AENDELEA KUSOTA RUMANDE KWA TUHUMA ZA MAUAJI




 Na Mwandishi Wetu Mara.


Kesi ya mauji ya kijana wankuru Nyamhanga mkazi wa Buriba Wilayani Tarime Mkoaii Mara inayomkabili Mfanyabiashara Wilayani Tarime imehairishwa kwa mara nyingine kutokana na upelelezi wake kutokamilika.


 Mfanyabiashara huyo anayefaamika kwa jina la  Lucas Sotel anatuhumiwa kwa  kosa la Mauji ya Kijana Wankuru Nyamuhanga ambayo yalitendeka Agosti  09 mwaka 2014 katika kijiji cha Buriba Wilayani Tarime.


 Mwendesha Mshitaka wa jeshi la Polisi Bukombe  Bukuru ameiambia Mahakama kuwa  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika nakupelekea kesi hiyo kupangwa tena Mnamo June 04  Mwaka huu.


Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Tarime Mh Veronica Mgendi ameharisha kesi hiyo ambapo  itatajwa tena  Maye Nne Mwaka huu.


Mtuhumiwa amerudishwa  Mahabusu mpaka upelelezi utakapokamilika  kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza  kesi inayomkabili Mfanyabishara huyo




Post a Comment

0 Comments