TANGAZA NASI

header ads

Kijiji cha Vanilla chafikiwa elimu ya moto,kudhibiti hasara ya mabilioni ya fedha

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania yenye changamoto kubwa ya tatizo la moto hususani kwenye majengo ya shule,hifadhi hata misitu kutoakana na shughuli mbali mbali  zikiwemo za kilimo mkoani humo.


Kwa kuliona hilo wataalam mbali mbali wameendendelea kutoa elimu ya moto ili kudhibiti hasara kubwa ambazo zinaweza kujitokeza mara baada ya changamoto hiyo.Ahmed Rizvi ni mmoja wa wageni kutoka jijini Dar es Salaam na mtaalamu wa maswala ya moto amefika mkoani Njombe na kutoa elimu ya kudhibiti moto katika kijiji cha Vanilla ili kuweza kuokoa hasara za mabilioni ya fedha yanayoweza kupotea.


“Zao hili ni jipya bado hapa Tanzania na kuna ujenzi mkubwa wa hizi Green house unaendelea Njombe kwa ghalama kubwa sana na hapa nikiangalia kwenye shamba utaona zao linategemea sana na haya majani,kwa hiyo ukiangalia haya mazingira akipita mtu anayevuta sigara anaweza kuleta madhara ndio maana tumetoa elimu kwa hawa vijana wanaoendelea na shughuli za kilimo kwenye huu uwekezaji”alisema Ahmed Rizvi


Ali Jawad ni miongoni mwa wageni waliofika ili kujifunza uwekezaji katika zao la Vanilla mkoani Njombe kutokana na zao hilo lenye ghalama kubwa kuendelea kukuwa kwa kasi mkoani humo.Amesema licha ya kuwa na shughuli zao ikiwemo kumilika taasisi za mashindano ya magari pamoja na kusaidia jamii lakini wamekuwa wakijihusiha katika kilimo na ufugaji hapa nchini ndio maana wamevutiwa pia katika kilimo cha Vanilla kinachoendelea mkoani Njombe.


“Tumependezewa hapa na kijiji cha Vanilla kwa kuwa tunajua kidunia ni zao namba mbili yenye ghalama baada ya Zafloo,na leo tumefika hapa na kutoa mawezo yetu na sisi kama wadau tuweze kuwekeza na pia kuvutia wawekezaji wengine”alisema Ali Jawad


Aidha ametoa rai kwa watanzani kuweza kujitokeza zaidi na kuweza katika zao hilo lenye bei juu duniani na imekuwa na uhaba katika upatikanaji wake kwa kuwa 80% ya zao hilo duniani inapatikana katika nchi ya Madagascar pekee.


“Asilimia 80 ya Vanilla inatoka Madagascar sasa kama Madagascar wanaweza kufanya hivi kwanini Tanzania Tushindwe, wakati tuna sehemu za joto tuna sehemu za baridi na sisi tunaweza kulima zao hili na kuwafikia wenzetu”alisema tena Ali Jawad


Saimon Mkondya ni mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla interneational inayojishughulisha na kilimo hicho katika mkoa wa Njombe ikiwemo kwenye kijiji kilichopewa jina la kijiji cha Vanilla kilichopo Idunda kata ya Yakobi.Ameshukuru watumishi wake kupata elimu ya kuepukana na majanga ya moto.


“Katika wageni wetu tuliowapokea tunashukuru pia tumempata mtaalamu wa kuzima moto,na ameweza kutufundisha jinsi ya kuepukana na majanga ya moto pamoja na kuzima katika hizi green house zetu,na ukizingatia zao hili ni ghali sana ambalo kilo moja inazidi milioni moja kwa hiyo moto ukitokea tutapata hasara ya mabilioni ya fedha”alisema Saimon Mkondya


Zaidi ya wageni 20 wamefika katika kijiji hicho cha Vanilla ili kujifunza namna kilimo hicho kinavyoendelea pamoja uwekezaji wake huku watumishi wa kijiji hicho 150 wakinufaika na elimu ya moto.

Post a Comment

0 Comments