TANGAZA NASI

header ads

WANAO CHOMA MOTO MISITU WAKABIDHIWA MIKONONI MWA WANANCHI

 





Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mbunge wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe Edwin Ennos Swalle ameagiza wananchi wa jimbo hilo kumchukulia hatua za haraka mwananchi yeyote atakayebainika anachoma moto msitu kuliko kusubiri katazo kutoka kwa viongozi wa kijiji ili kulinda mazingira na mali zinazotokana na misitu.


Ameeleza hayo alipokuwa kwenye ziara kata ya Kidegembye tarafa ya Lupembe huku akitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha kiangazi ili kuepuka kutokea kwa matukio ya moto katika tarafa hiyo kwani matukio hayo yamekuwa yakiharibu rasilimali misitu katika jimbo la lupembe.


“Ukichoma msitu mmoja wa miti unapoteza fedha nyingi sana,kwa hiyo ukimuona mwananchi mwenzako anachoma moto bila utaratibu usisubiri mwenyekiti wa kijiji aje kumkataza,tuchukue hatua ili tulinde mazingira na mali yetu ambayo ni miti”alisema Swale



Pamoja na wito huo kwa wananchi wa jimbo hilo ameonya  kuhusu uuzaji wa ardhi kiholela.


“Tunzeni vizuri ardhi yenu,unaweza ukauza ardhi yote ukaona hata pa kujenga choo hamna,Ardhi ni maisha na ardhi ndio kila kitu”Alisema tena Swalle


Mwenyekiti wa kijiji cha Image  Ferix Payovela naye ametoa wito kwa wananchi.

“Ninaomba wananchi mlizingatie hilo agizo la juu ya matumizi bora ya ardhi “alisema Ferix Payovela



Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kidegembye pamoja na kijiji cha Image akiwemo Lodrick Mhada wamekieleza kituo hiki kuwa matukio mengi ya moto yanatokana na uzembe wa wananchi wakati  wa urinaji wa aridhi.

“Pia tuna kamati yetu amabyo kila mtu anapotaka kwenda kuchoma moto lazima akaripoti ofisini ndipo anaruhusiwa kwenda na watu wasiopungua 10 kwenda kuchoma moto mashamba”alisema Lodrick Mhada


Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale amefanya ziara katika kijiji cha Kidegembye pamoja na kijiji cha Image ambapo amesisitiza utunzaji bora wa aridhi pamoja na kuepuka uchomaji moto ovyo katika jimbo hilo.


Post a Comment

0 Comments