TANGAZA NASI

header ads

Serikali kujenga hoteli tano za kitalii hifadhi ya wanyama pori ya Mpanga-Kipengere

 

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Serikali nchini Tanzania inakusudia kuboresha miundombinu katika hifadhi za kitalii ikiwemo barabara na hoteli ili kuweka mazingira rafiki kwa watalii na kuongeza mapato serikalini kupitia wizara ya maliasili na utalii.


Katika utekelezaji wa mpango huo katika hifadhi ya Mpanga-Kipengere iliyoko kusini magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Njombe ndani ya hifadhi hiyo inatarajiwa kujengwa hoteli tano za kitalii.



Hifadhi ya mpanga kipengere imeanza kupata watalii wa ndani na nje kufuatia uwepo wa vivutio mbalimbali maarufu ikiwemo pango linaloelezwa kwamba alilojificha chifu wa Wahehe Mkwawa wakati wa vita ,maporomoko ya maji zaidi ya saba na na miamba ya aina mbalimbali.


"Katika hifadhi hii tumetenga maeneo matano kwa ajili ya uwekezaji wa hoteli za kitalii,eneo la Kimani tumetenga maeneo matatu,Ikovo tumetenga eneo moja na Ibaga eneo moja"alisema Ambrosy Mng’ongo ni Kamishna msaidizi mwandamizi TAWA.


Baadhi ya watalii waliofika katika hifadhi hiyo kujionea mazuri yaliyopo ni mkuu wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Reuben mfune ambae amezungumzia vivutio vilivyomo katika hifadhi hiyo.



"Nimefika eneo ambalo Mkwawa alikuwa analitumia kwa ajili ya shughuli za kuoga na kuna sehemu ambayo alifnay kama makazi amabayo ni pango lilioundwa kwa jiwe na hapo kuna viti vinne ambavyo aliviacha kwa wakati ule"alisema Reubeni mfune Mkuu wa wilaya ya Mbarali


Naye Moses Nsata mtalii wa ndani alisema"Kikubwa kilichonifurahisha kwanza ni mazingira halisi,tunaomba watanzania waendelee kutembelea vivutio vyao"alisema Moses Nsata



Kaimu meneja wa hifadhi ya mpanga kipengere Alfred Pondamali amesema tayari serikali imesha fanya ukarabati wa barabara kwa kilometa 13 kutoka barabara kuu ya Makambako - Mbeya sambamba na ujenzi wa vyoo katika eneo la hifadhi.


"Yamenza maboresho katika ujenzi wa barabara ambayo liko kwenye bara bara kuu katika kijiji cha Kimani kwenda Mbeya"alisema Pondamali

 

Hifadhi ya mpanga kipengele hifadhi iliyoko katika mkoa wa Njombe ikiwa ni miongoni mwa hifadhi zilizo chini ya mamlakaya hifadhi za Wanyamapori Tanzania TAWA.

Post a Comment

0 Comments