Na Amiri Kilagalila,Njombe
Watu wawili wanashikiliwa na vyombo
vya dola mkoani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi na
mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana
wa CCM (UVCCM) vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Iringa Emmanuel Mlelwa aliyeuawa na
kutambuliwa siku 6 baada ya kifo chake.
Akizungumza katika mazishi
yaliyofanyika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa,mkoani Njombe.Mkuu
wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya.amesema watu wawili wanashikiliwa kwa
tuhuma za mauaji hayo huku wakiendelea na upelelzi wa awali.
Aidha amewata wananchi kuwa
wavumilivu kwa sasa kwa kuwa vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi ili
kuwabaini waliohusika na mauaji hayo
“Sasa hivi tupo katika kampeni kwa
maandalizi ya uchaguzi mkuu,lakini kampeni haiwezi ikatumika kuvunja amani.Kama
alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,tutawasaka wahusika kwa
nguvu zote kuhakikisha wametiwa mbaroni”alisema Marwa Rubirya mkuu wa mkoa wa
Njombe
Vile vile aliema “Maendeleo
mnayoayaona katika nchi yetu yanaonekana kwasababu tuko katika mazingira ya
amani,niwaombe wakati serikali tunapoendelea kushughulika na jambo hili
niwaombe wananchi tuendelee kuonyesha ukomavu kuhimili jambo hili” aliongeza Marwa
Rubirya
Amewathibitishia wananchi kuto
kuachwa yeyote atakayebainika kuhusika na mauaji hayo “Niwathibitishie kuwa
hakuna aliyehusika na uhalifu huu,ambaye hata chukuliwa sheria kwa mujibu wa
sheria za nchi yetu”
Nao chama cha Mpainduzi CCM mkoa wa
Njombe kupitia kwa mwenyekiti wake Jassel Mwamwala kimewataka vijana kuendelea
kuwa watulivu kwa kuwa serikali inaendelea kulifanyia kazi swala hilo.
“Na ninny vija tunaomba tulieni
acheni mihemko serikali yetu inafanya kazi na hakika tutapata jibu”alisema
Mwamwala
Kijana huyo ameuawa kikatili wiki
lililopita na watu wasiojulikana na mwili wake kutambuliwa baada ya siku sita
ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mji wa Njombe
kibena
Marehemu Emmanuel Mlelwa alihudumu
kama mwenyekiti wa wanafunzi wa CCM wa vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Njombe kabla
hajahamia mkoa wa Iringa ambako nako alikuwa akihudumu kwa cheo hicho akiwa
mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumain kabla mauti hayajamkuta wakati akiwa
likizo.
0 Comments