Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Serikali Wilayani Njombe
imeongeza muda wa siku nne kuanzia leo za kutuma maombi kwa ajili ya kujiunga
na nafasi za jeshi la kujenga Taifa (JKT) kutokana na vijana kutojitokeza kwa
wingi mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya
Njombe Bi.Ruth Msafiri amesema zoezi hilo
lilitakiwa kukamilika septemba 9 mwaka huu na kutokana na idadi ndogo ya
vijana waliokwenda kuomba, serikali imeongeza muda huo wa siku nne hadi tarehe
11 .
“Tarehe yetu ya
mwisho ya kupokea tulikuwa tumepanga iwe tarehe 9 saa kumi jioni ambayo ni
kesho,lakini mimi nimefungua na nitaendelea kupokea majina ya waombaji wote na
vikao vyangu nitafunga rasmi tarehe 11”alisema Ruth Msafiri
Aidha Bi.Msafiri
amesema vijana wenye sifa ya kujiunga na JKT ni wenye elimu ya darasa la saba
hadi chuo kikuu ambapo vijana 130 wanahitajika kujiunga na jeshi hilo.
“Kwa kuwa lengo ni
kupata vijana wa kutosha kupata fani na stadi mbali mbali za maisha,hii
inahusisha madarasa yote kwa maana elimu ya msingi,sekondari,kidato cha sita,cheti,lakini
pia hata wa chuo kikuu”aliongeza DC Msafiri
B.Msafiri ametumia
fursa hiyo kukemea tabia za baadhi ya watu wanaotaka kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu kupitia zoezi hilo
kinyume na sheria ambapo kwa atakaye bainika hatua kali zitachukuliwa.
“Hizi nafasi
hazitolewa kwa upendeleo wa aina yeyote,wewe ukitoa rushwa utakuwa
umeumizwa,mimi sitoi hiz nafasi kwa upendeleo kwasababu sio za mfukoni ila
tunakwenda nazo kwa sifa”alisema Ruth Msafiri
Kituo hiki
kimezungumza na baadhi ya vijana mjini Njombe wamesema wanatambua kuwepo
umuhimu wa kujiunga na JKT ikiwemo kujengewa uzalendo na kulilinda Taifa.
0 Comments