Makete
Wananchi wa kijiji cha Usagatikwa kata
ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wamewaomba viongozi watakaochaguliwa
katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu kwa nafasi ya udiwani wa kata hiyo
na ubunge wa jimbo la Makete, waweze kuwaunga mkono juu ya mpango wa ujenzi wa
zahanati ya kijiji hicho.
Wananchi hao Akiwemo Sioni Sanga na
Abigo Albon Sanga wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na kituo hiki ambapo
wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kijiji hicho kuwa na zahanati kutokana na
umbali uliopo kufika katika hospitali ya Consolatha Ikonda ambayo kwa sasa
ndiyo wanayoitegemea kupata huduma.
Mwl Linusi Ally Vangamea wa Shule ya
Msingi Usagatikwa ameungana na wananchi wa kijiji kicho kulilia kuwepo kwa
Zahanati Kijijini hapo ili Kuepusha Usumbufu kwa wanafunzi Kusafiri mpaka
Kijiji cha Jirani kupata Huduma.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Usagatikwa
Bi.Lucy Valentino Lukinga amesema tayari wameshafyatua tofali na wanatarajia
kuanza kuzichoma wiki ijayo huku akiwataka wananchi waendelee kushirikiana na
viongozi wao ili waweze kufanikisha ujenzi huo.
0 Comments