TANGAZA NASI

header ads

Mkenge alilia Chuo Cha Ufundi Bagamoyo



Na Omary Mngindo, Bagamoyo


MGOMBEA Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge, amesema kuwa alipokuja Mgombea Mwenza wa Urais Mama Samia Suluhu, alimkabidhi ombi la ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) ili vijana wapate ujuzi.


Sanjali na VETA pia Mkenge alisema ameiomba Serikali kukiangalia kipande cha barabara kutoka Daraja la Makofia mpaka Sunguvuni kuelekea Mashine ya Maji Ruvu chini, ili magari yanayopeleka dwa yapite kwa vipindi vyote.


Mkenge aliyasema hayo katika mkutano wake wa kwanza wa Kampeni kwenye uwanja wa Mgonela Kata ya Dunda jimboni hapa, ambapo alisema Chuo Cha Ufundi kitakuwa suruhisho kwa vijana kuajiliwa kwenye viwanda, kujiajili wenyewe sanjali na kuajili wenzao.


"Nilimkabidhi kilio cha ujenzi wa barabara ya Makofia mpaka Sunguvuni, ili kuyawezesha magari yanayopeleka dawa kwenye chanzo cha maji cha Ruvu chini yaende wakati wote, mwaka huu magari yalikwama kwa mvua, pia ifike mpaka Mlandizi," alisema Mkenge.


"Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ni sikivu, kama tutakumbuka miaka mitano iliyopita mgombea weyu wa Urais Dkt. John Magufuli alipokuja kuomba kura kaka yangu Dkt. Shukuru Kawambwa alimuombaa kilometa tano za lami tayari zimeshajengwa," alisema Mkenge.


Mkenge aliongeza kwamba alipowasilisha maombi hayo Mama Samia aliwaambia kwamba katika utekelezaji wa Ilani 2020/2025, barabara ya Makofia Mlandizi itajengwa kwa kiwango cha lami, sanjali na kulipwa fidia kwa wananchi wataopitiwa na mradi huo.


Aidha aliishukuru Serikali kwa ujenzi wa Vituo vya afya viwili vilivyojengwa Matimbwa Kata ya Yombo na cha Mapinga, ambapo cha Mapinga kimeshaanza kuwapatia huduma wagonjwa wanaofika kwa ajili ya kupata tiba.


"Serikali ya CCM inapoahidi inatekeleza, mwaka 2015 kaka yangu Dkt. Shukuru Kawambwa alimuomba mgombea Urais mwaka huo Dkt. John Maguguli barabara ya lami kilometa 5, zimejengwa nami nikamuomba Mama Samia atuongezee kilometa tano nyingine," alisema Mkenge.


Kwa upande wake Mbunge aliyemaliza muda Dkt. Shukuru Kawambwa alisema kuwa anaimani na Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Magufuli, huku akisema kuwa Oktoba 28 akichaguliwa asimamie mchakato wa ujenzi wa Kituo cha afya barabara ya Bagamoyo Msata eneo la Fukayosi.


"Serikali ilitupatia pesa tukajenga Vituo vya afya Kerege na Matimbwa pia tukawa na mpango wa ujenzi mwingine  Kata ya Fikayosi, nikuombe utakapochaguliwa simamia hilo, tunataka barabara zetu kubwa tatu zote ziwe na Vituo vya afya," alisema Dkt. Kawambwa.


Awali Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa Alhaj Abdul Sharifu aliwataka wana-Bagamoyo kumchagua kwa kura za kishindo mhonbea urais Dkt. John Magufuli, Muharami Mkenge, Apsa Kilingo na madiwani wote wanaotokea chama hicho.


Post a Comment

0 Comments