Na Amiri Kilagalila,Njombe
Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe
kimewatangazia wananchi ratiba na mapokezi ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh,Samia Suluhu Hassan,ambaye pia ni mgombea mwenza wa
kiti cha Urais 2020 anayetarajia kupokelewa mkoani humo katika wilaya ya Ludewa
September 18 akitokea mkoa wa Ruvuma.
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM
Mkoa wa Njombe Erasto Ngole mbele ya waandishi wa habari amefafanua ratiba ya
mapokezi wa kiongozi huyo wa kitaifa
“Mgombea mwenza wa kiti cha Urais Mh,Samia Suluhu
Hassan ataingia kwenye mkoa wetu tarehe 18 mwezi huu wa tisa na atatokea Ruvuma
kupitia wilaya ya Ludewa na tarehe 19 atakuwa kwenye mkutano mkubwa wa kampeni
kwenye kata ya Mlangali” amesema Erasto
Ngole alisema tena
“Makamu wa Rais (Mgombea mwenza) tarehe 20 majira ya
mchana atakuwepo wilaya ya Njombe na atafanya mkutano mmoja tarafa ya Lupembe
eneo la Wanginyi kwa hiyo wananchi wote wa jimbo la Lupembe wajue Makamu wa
Rais atafanya mkutano katika maeneo yote” alisema Erasto Ngole
Vile vile alisema Makamu wa Rais atamaliza kampeni
mkoa wa Njombe kupitia wilaya ya Makete mkoani humo
“Tarehe 21
mwezi huu 9 Makamu wa Rais (Mgombea mwenza) atafanya mkutano mkubwa sana kwenye
uwanja wa Sabasaba eneo la Iwawa,Makete mjini.Wananjombe wajue mkoa wetu
utatembelewa na wagombea wa Chama chetu cha Mapinduzi kwa hiyo baada ya Samia
tutawatangazia pia ratiba ya Mh,Rais” Erasto Ngole katibu
Aidha bwana Ngole ametangaza amewatangazia wananchi
uzinduzi wa kampeni za siasa kimkoa utakaofanyika hapo kesho Septemba 9/2020
“Kesho tarehe 9 mkoa wa Njombe unafanya uzinduzi wa
kampeni kimkoa,na uzinduzi huu utafanyika viwanja vya polisi halmashauri ya mji
wa Makambako,Wanaccm wote tunatakiwa kuhudhuria sherehe hizi tukiwa katika
mavazi ya Chama,na wasanii wote mkoa wa Njombe wanaalikwa na watapata nafasi ya
kuburudisha” Erasto Ngole
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wanachama na
viongozi kuendelea kutafuta kura kata kwa kata katika maeneo yao
“Huu ni muda wa kutafuta kura,tunaendelea kuwaomba
wagombea wetu waendelee kufanya kampeni za ndani kwa kuwa ni muhimu sana,waende
kwenye ngazi ya mashina kwa maana ya nyumba kwa nyumba,mtu kwa mtu ili tuweze
kushinda kwa kishindo” alisema Erasto
0 Comments