Na Fredy Mgunda, Iringa.
WANANCHI wa jimbo la Mufindi Kusini wanamatarajio ya kutatuliwa kero ya miundombinu ya barabara na maji kutokana na ahadi ya mgombea ubunge wa jimbo hilo alipokuwa akiomba kura za kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Akijinadi mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Igowole kata ya Igowole, Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kusini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) David Kihenzile alisema kuwa tatizo la ubovu wa barabara limekuwa sugu kwa miaka mingi na kusababisa madhara makubwa ya kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.
Alisema kuwa miundombinu ikiwa bora inasaidia kukuza uchumi wa wananchi kutokana na shughuli za kimaendeleo ambazo zinakuwa zinafanyika katika maeneo ya vijiji au miji ya kibiashara hasa usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali.
“Kukiwa namiundombinu bora kunarahisisha kuboresha sekta ya elimu,afya na kilimo kwa kusaidia kurahisha usafi kwa wananchi wanaopenda kufanya shughuli za kimaendeleo”alisema Kihenzile
Kienzile alisema kuwa jimbo hilo linakabiliwa na changamoto nyingine ya maji iliyodumu kwa miaka mingi na kupelekea kudhofisha ukuaji wa uchumi kwa wananchi hivyo ni lazima kuhakikisha anatafuta njia ya kutatua changamoto hiyo.
“Ukikosa maji katika maisha ya wananchi yeyote unakuwa umeharibu maisha yake, hivyo mkinipa ridhaa ya kuwa mbunge wenu nitahakikisha natafutia njia ya kutatua changamoto hiyo ya kero ya maji” alisema
Aidha kienzile aliwatoa hofu wananchi kuhusiana swala ya kuboresha sekta ya afya kwa kuwa analitambua hilo na alishaanza kulifanyia kazi kabla ya kuanza kugombea ndio maana alitafuta vifaa vya zaidi ya bilioni moja ambavyo vinasaidia kutibu wagonjwa.
Lakini Kihenzile amesema vijana na wasomi wote wanaoishi nje ya Mufindi wanapaswa kurudi nyumbani na kuijenga Mufindi kimaendeleo.
Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Igowole kata ya Igowole wilayani Mufindi.
Kihenzile alisema atajitahidi vijana wenye uwezo wanaotokana na jimbo la hilo kukumbuka na kurudi nyumbani kuijenga Mufindi yao.
“Wapo wenzetu wa Mufindi wapo katika nafasi kubwa na wengine wameaminiwa serikalini hivyo tuwatumie na wao wakumbuke kurudi kuijenga Mufindi yao ili kiwasaidia wananchi wanaoishi Jimboni kuona manufaa ya watoto wao waliowasomesha na kupata ajira nje na ndani ya Iringa”alisema
Alisema wapo vijana wengi katika jimbo hilo wana ajira wanauwezo na wanauzoefu na wengine hawana uzoefu tutajitahidi kuwatambua wako wapi hata kama wapo nje ya Mufindi tutahakikisha tunahangaika kutafuta fulsa za kuwa saidia ndani ya Jimbo
0 Comments