Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi,Ruth Msafiri amesema
jeshi la kujenga Taifa (JKT) katika mwaka wa 2020/2021 limetoa nafasi za
nyongeza kwa vijana waliohitimu darasa la saba na kidato cha nne tu,kujiunga na
mafunzo kwa mkataba wa miaka miwili kwa utaratibu wa kujitolea na maombi hayo
yakianza kupokelewa hii leo mpaka hapo kesho Mei 6,2021.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa taarifa hiyo wakati
akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwakwe huku akitoa wito kwa vijana
wanao hitaji na wenye sifa za kujiunga na jeshi hilo kufuata utaratibu ili
waweze kujiunga kupitia nafasi hizo.
“Sifa ni zile zile za siku zote kwanza ni lazima awe
raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 16-18 kwa vijana wenye elimu ya darasa
la saba,huku vijana wenye elimu ya kidato cha nne awe na umri usio zidi miaka
20”Alisema Ruth Msafiri
Amesema sifa zingine ni pamoja na “Awe na afya
njema,akili timamu na asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo),vile
vile awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri na hajapatikana na hatia
mahakamani wala kuwahi kufungwa”alisema Msafiri
Kuhusu uafaulu wa kijana anayehitaji kujiunga na
jeshi hilo mkuu wa wilaya amesema. “Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari safari
hii wamekuja na uafaulu,kidato cha nne wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2018,2019
na 2020 wenye ufaulu wa daraja la tatu na la nne (Div.111 na Div 1V) na
hawajatuambia poit”alisema Ruth Msafiri
Hata hivyo amesema ni muhimu vijana hao kuwa na
uthibitisho wa kuhitimu elimu ya msingi pamoja na cheti halisi cha kuzaliwa
huku wale waliomaliza kidato cha nne ni muhimu kuwa na cheti halisi cha
kumaliza shule.
Vile vile Msafiri amesema nafasi hizo na kwa vijana
wasio wahi kutumikia jeshi la polisi
“Awe hajawahi kutumika jeshi lolote liwe jeshi la
polisi,Magereza,chuo cha mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na idara nyingine
serikalini na asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma kwasababu kuna wengine
wakiskia nafasi wanarudi tena”alisema Msafiri.
Amesema barua za maombi hay ohayo zinapaswa
kupitishwa kwa maafisa watendaji wa kata au kijiji husika anapoishi mwombaji
ili kuthibitisha ukaazi wake huku zikiwa zimeambatanishwa na vivuli vya vyeti
vinavyohusika katika maombi na kuwataka viajana kuchangamkia fursa hiyo
inayotarajia kuanza usaili Mei 7 mwaka huu.
MAELEZO YA PICHA
A:Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akitangaza
nafasi hizo za nyongeza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii
leo.
B:Picha ya mtandaoni inayoonyesha baadhi ya vijana
waliowahi kujiunga na JKT


0 Comments