TANGAZA NASI

header ads

Wamiliki wa viwanda mkoani Njombe wafikiwa na elimu ya matumizi bora ya umeme

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko,limeendelea kutoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa viwanda  na wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa mkoani Njombe ili waweze kufahamu  jinsi ya kupunguza gharama ambazo si za lazima kwa kununua vifaa vya kisasa  na kuachana na vifaa vilivyochakaa na vya zamani kwani vinatumia umeme mwingi.


Team ya TANESCO kutoka makao makuu iliyoambatana na afisa masoko Bi,Jennifer Mgendi na TANESCO mkoa wa Njombe wamekutana na baadhi ya wamiliki hao na kuwafikishia elimu kuhusu utaraibu wa kufunga motor za kisasa na kuzifanyia service mara kwa Mara ili motor iendelee kuwa na ufanisi.


Aidha wametoa elimu ya usalama wa umeme kwa kuwa nishati hiyo ni nzuri pia umeme ni hatari kutokana na madhara yanayoweza kutokea baada ya kuwaka moto unaotokana na sababu mbali mbali.


Vile vile wataalamu hao wametoa elimu ya kufunga power factor ili iweze kuwasaidia katika uendeshaji wa mitambo yaani KVA haitakuwa kubwa.


Wamiliki hao pia wameelezwa faida ya matumizi bora ya umeme ukiwa ni pamoja na kuokoa pesa yao.


Ezekiel Chaula ni mmoja wa wamiliki wa viwanda vidogo anayetumia umeme katika shughuli zake za uchomeleaji katika kata ya Ilembula wilayani Wanging'ombe amewashukuru Tanesco kwa elimu hiyo huku akiomba elimu iwe endelevu


"Kwanza niwashukuru Tanesco kwa huduma zao wanazozitoa tofauti na kipindi cha nyuma.Changamoto tunazokutana nazo sasa hivi ni za kawaida na kadri siku zinavyozidi kwenda zinazidi kuboreshwa"alisema Chaula


Ameongeza kuwa "Kwasasa hata kama umeme unakatika kwa dharula tunapewa taarifa mapema sana na kujiandaa tofauti na hapo awali"aliongeza Chaula


Viwanda vilivyotembelewa mkoani Njombe hususani katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe na Njombe ni pamoja na mashine za kusaga na kukoboa,bakery na viwanda  vidogo vya kukamua alizeti.

Post a Comment

0 Comments