TANGAZA NASI

header ads

Mkenge akabidhi futari kwa makundi maalumu

 



Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge, kupitia Katibu wake Zainabu Kihate amekabidhi futari katika taasisi na makundi maalumu, ikiwa ni sadaka yake katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Futari hiyo iliyosambazwa na Katibu huyo imezihusu taasisi mbalimbali ikiwemo shule za sekondari na Jeshi la Magereza Kigongoni lililopo Kata ya Magomeni jimboni hapa, ambapo walengwa wakuu ni wafungwa na Mahabusu.

Shule za sekondari zilizonufaika na sadaka hiyo ni Zamzam na Miembesaba zilizopo Kata ya Yombo, Dunda, Bagamoyo na Kingani ambapo katika maeneo yote Kihate aliwasilisha salamu za mbunge huku akiwatakia mfungo mwema wa mwezi wa ramadhani.

"Kwa niaba ya Mbunge wa Bagamoyo Muharami Mkenge, nimefika hapa kuwakabidhi futari kidogo itayoweza kutusaidi japo kwa siku moja, mbunhe alitamani kuwakabidhi kikubwa zaidi lakini uwezo wake umefikia hapa, naomba mkipokee kwa uchache huu," alisema Kihate.

Aliongeza kwamba mbunge amewatumia salamu za mfungo wa mwezi wa ramadhani, huku akieleza kwamba mara baada ya bunge la bajeti litakapomalizika akirejea jimboni atafika katika taasisi hizo kuwasalimia, lakini pia kuwashukuru kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM.

"Nimefika hapa kwa ajili ya ziara kutembelea makundi yenye uhitaji maalumu, wakiwemo wazee wasiojiweza, yatima, wananchi walio katika mazingira magumu pamoja na wanafunzi kwenye shule za sekondari," alisema Katibu huyo.

Wakitoa shukrani kwa Katibu huyo kwa niaba ya Mbunge Mkenge, baadhi ya wanafunzi Masunga Masunga, Rehema Issa wa sekondari ya Bagamoyo na mwalimu Samuel Chritian wa sekondari ya Dunda walimshukuru mbunge huyo, huku wakisema sadaka hiyo haina udogo.

"Tufikishie salamu kwa mbunge wetu Mkenge, mwambie tunampenda sana pia tunamuombea aendelee kuwa na afya njema ili atutumikie wapigakura wake," alisema mwalimu Christian.

Post a Comment

0 Comments