TANGAZA NASI

header ads

Mahakama yamkuta na hatia Mwenyekiti wa Kijiji




 Na John Walter-Kiteto.

Mahakama wilayani Kiteto mkoani Manyara imemkuta na hatia Mwenyekiti wa kijiji cha Njoro Omari Jumbe aliyekuwa akishtakiwa na Takukuru kesi namba cc. 48/2020 kwa makosa manne ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki tano ili aachilie mifugo aliyokuwa ameikamata.

 Mahakama hiyo chini ya Mheshimiwa Hakimu Joakimu Mwakyolo imempa adhabu ya kulipa faini ya shilingi laki tano kwa kila kosa au kwenda jela miaka mitatu ambapo aliweza kulipa jumla ya shilingi jumla ya shilingi mbili hivyo kukwepa kutumikia kifungo.

Kesi iliendeshwa na wakili Yahya Masakilija kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).

Post a Comment

0 Comments