Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mgombea wa udiwani wa kata ya Wailes, halmashauri ya manispaa ya Lindi kupitia chama cha Alliance for Change and Transparency ( ACT- Wazalendo), Abdallah Faustine amesema kitendo cha serikali kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa ndicho kilichosababisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kifanye kazi ngumu ya kujibu hoja za wapinzani katika kampeni zinazoendelea.
Faustine aliyasema hayo jana wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mtaa wa Muhimbili, kata ya Rasbura, manispaa ya Lindi.
Mgombea huyo ambae alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi katika mkutano huo kwa ajili ya kuwanadi mgombea ubunge wa jimbo la Lindi, Isihaka Mchinjita na wa udiwani wa kata ya Rasbura, Abass Ng'wachi alisema kitendo cha serikali kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa kimesababisha CCM kitumie muda mwingi kujibu hoja za wagombea wa vyama vya upinzani badala kunadi ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020.
Alisema CCM kisingekuwa na kazi ngumu iwapo serikali isingewafunga midomo wanasiasa wa vyama vya upinzani. Kwani kingejibu hoja kila ilipobidi kufanya hivyo kwawakati. Kwahiyo kingeingia kwenye uchaguzi kikiwa kimepangua hoja nyingi au kuikemea serikali irekebishe kasoro. Hivyo kwenye kampeni za uchaguzi kingejikita kueleza utekelezaji wà ilani yake ya 2015-2020 na kueleza mazuri yaliyopo kwenye ilani ya 2020-2025.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano serikali ilikosa mawazo mbadala kutoka kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao kimsingi ni jukumu lao na msaada wao kwa serikali. Badala yake ilifanya mambo bila kupokea ushauri. Hali aliyodai imesababisha kuharibu mambo mengi ambayo CCM kinapata shida kujibu kwa wananchi baada ya viongozi na wagombea wa vyama vya upinzani kukishataki kwa wananchi hao.
" Inawezekana baadhi ya mipango ilikuwa mizuri na yenye tija kwa taifa. Lakini utekelezaji wake ukawa mbovu. Wale ambao wangewashauri walizibwa midomo na ikajiona inafanya vizuri. Kumbe kuna maeneo mengi imeharibu ingawa kipindi chote cha miaka mitano ilifanya kazi ya kujisifu. Wanashindwa kujibu hoja za wapinzani wanajjkuta wanahaidi kufanya ambayo hayapo kwenye ilani yao ya 2020 bila kupenda," alisema Faustin.
Alikiri kwamba serikali imefanya ambayo yanaonekana kuwa ya maendeleo. Hata hivyo mengi kati ya hayo hayana faida kutokanana mahitaji ya wananchi yanayosababishwa na wakati husika. Kwamadai kwamba baadhi ya miradi kama reli ya kisasa, ndege na barabara za juu siyo mahitaji ya wananchi kwasasa.
" Hivyo vyote ni muhimu kwa maendeleo.Bali umuhimu wa kitu unatokana na mahitaji ya wakati husika. Mwenye kiu ya maji ukimpelekea ugali hawezi kukuelewa japokuwa ugali pia ni muhimu. Mpe maji anywe ndipo mpe chakula. Ukimlazimisha ale ugali atakufa kwakiu na hakuna atayekusifu kama wewe ni mwema ataukijisifu. Hayo hayakuwa mahitaji ya wananchi ambao wanaishi bila kujua hatima ya walau ya maisha yao ya kesho kuhusu uhakika wa kula na matibabu. Kwanini wasiongeze bajeti ya kilimo ili wakulima wazalishe kwa wingi? alisema Faustin.
Aidha mgombea huyo wa udiwani alisema umefika wakati wakuchagua watu wenye mawazo na mitazomo mipya kuhusu namna ya kuinua jimbo na manispaa ya Lindi kimaendeleo. Kwamadai kwamba ukongwe, historia na umaarufu wa mji wa Lindi haufanani na ulivyo.
Alisema majengo mengi ikiwamo ya ghorofa yanayoonekana katika mji huo yalijengwa zamani na wazee. Nikutokanana wakati huo kuwepo harakati na shughuli nyingi za kiuchumi. Lakini hali hiyo nitofauti na sasa. Kwani shughuli za kiuchumi zimedorora kiasi chakusababisha wasomi wengi kukimbia mji huo. Kwamadai kwamba mji huo sio rafiki kujiajiri.
Alisema vijana wengi wa Lindi ambao wanaelimu kubwa wanashindwa kubaki katika mji huo.Japokuwa ipo dhana kwamba watu wa mji huo wajasoma, bali ukweli nikwamba wanashindwa kuishi kutokana kudorora shughuli za kiuchumi.
Kufuatia hali hiyo aliwataka wananchi wa kata hiyo na jimbo la Lindi wawachague wagombea wa upinzani ambao wana mawazo mbadala. Badala ya CCM ambayo alidai kuwa imesababisha hali ngumu ya maisha na kuchakaza mji wa Lindi.
Kwaupande wake mgombea uunge wa jimbo la Lindi, Isihaka Mchinjita alisema akichaguliwa na kuwa mbunge atapambana kutatua changamoto ya barabara na zahanati katika mtaa huo na kata ya Rasbura.
0 Comments