Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amesema uendeshaji wa ATCL hauingiliwi bali inajiendesha yenyewe kwa kuzingatia sheria na kanuni iliyoianzisha.
" Tuache kuwapotosha wananchi bali tusifu utendaji kazi mkubwa wa Rais Magufuli kwa kuleta ndege zilizorahisisha usafiri, kuchochea shughuli za kiuchumi, utalii na kilimo kwa kuweka miundo mbinu bora ya usafirishaji wa mazao ambayo ni perishable.
Nyie wapotoshaji angalieni zile hotuba za yule kidudu mtu alisoma Bungeni kuwa ATCL bajeti yake ipo chini ya Uchukuzi fungu 62 na akajadili manunuzi ya ndege, hizi akili za vidudu mtu tuziache , hapa ni mbele kwa mbele ndege ziataendelea kununuliwa katika kuchangia ukuaji wa uchumi," Amesema Ditopile.
Amewaomba watanzania kuepuka wapinzani ambao wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kupinga mafanikio katika sekta ya anga licha ya kwamba wao wenyewe wamekua mstari wa mbele kupanda ndege za shirika la ndege la ATCL.
0 Comments