MAKAMBAKO
Wakazi mjini Makambako mkoni Njombe wanataraji
kuondokana na changamoto ya uhaba wa maji ifikapo Octoba mwaka huu baada ya
serikali kupitia mamlka ya maji mjini humo MAKUWASA kukamilisha ujenzi wa mradi
wa bwawani ulionza kujengwa tangu mwaka 2017 pamoja na tank la maji la lita
laki moja.
Hayo yamebainishwa na Eng Fabiani Maganga msimamizi
wa miradi ya maji inayojengwa kutika mikoa ya njombe na Iringa wakati kamati ya
kusimamia miradi hiyo kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira ya mjini
iriga IRUWASA ikiwa katika ziara ya kukagiua miradi hiyo katika mkoa wa Njombe.
Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa
mazingira mji wa makambako MAKUWASA Osca Lufyagile amesema kuwa kukamilika kwa
mradi huo kutasaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa maji ambapo kwa
sasa wakazi wa mji huo wanapata maji kwa mgao kila baada ya siku tatu na
kueleza mipango ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji kutoka mito ya safu za milima
kipengere.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na
usafi wa mazingira mji wa Iringa IRUWASA Gilbert Kayange ameitaja miradi
ambayo bodi ya mamlaka hiyo inaisimamia kwa mikoa ya njombe na Iringa na kuwa
iko katua hatua za mwisho kukamilika.
0 Comments