TANGAZA NASI

header ads

Watoto zaidi ya milioni mbili kuokolewa dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa



Na Frankius Cleophace Mwanza


 Zaidi ya watoto Milioni Mbili hadi tatu  kila mwaka wamezidi kuokolewa  duniani dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa  kwa kupatiwa chanjo za aina mbalimbali.  


Kauli hiyo imetolewa na Dk :Leonard Subi ambaye ni mkurugenzi wa kinga Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na watoto Katika semina ya waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Mwanza, Shinyanga Simiyu na Mara  yaliyofanyika jijini Mwanza.


Dk: Leonard alisemakuwa Wizara ya Afya mnamo mwaka 1975 ilianzisha  mpango wa taifa wa chanjo kwa ajili ya kuboresha maisha na ukuaji wa watoto ambapo zilianishwa chanjo mbili na hadi sasa zimefikia chanjo  aina tisa ambazo zinakinga magonjwa kumi na tatu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.


Dk: Leonard aliongeza kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha inatokomeza vifo visivyo vya lazima vinavyotokana na milipuko ya magonjwa mbalimbali kutokana na ukosefu wa chanjo mbalimbali kwa watoto wadogo.


 Vile vile Dk: Leonadrd amewasihi wazazi na walezi kupeleka watoto wote ili kuweza kupata chanjo ili kuendelea kuwa na kinga mwilini kwa lengo la kuepuka magonjwa ya kuambukiza.


 “ Ikumbukwe chanjo inatolewa na serikali tu na vituo vya binafsi ambavyo tumevipa mamlaka nasisitiza pia  waganga wakuu wote  wa  mikoa Nchini wahakikishe kila mtoto anayestahili aweze kupatiwa chanjo wanahabari wasikilize wataalamu ili mwendelee kuelimisha jamii juu ya masuala mazima ya chanjo chanzo zote ni salama”  alisema Dk Leonard.


 Pia Dk: Leonard amesisitiza  kuwa serikali imeendelea kutoa bajeti za kutosha kwa ajili ya kuboresha mpango wa chanjo ambapo mwaka  2014-2015 bajeti ya chanjo imetoka bilioni 10 hadi Bilioni 30 mwaka 2019-2020 hadi 2021.


 “Tumeweza kufanya ukarabati  maghala ya kuifadhia chanjo  ambapo yameghalimu pia Bilioni 1.3 pia vyumba vya ubaridi vimeghalimu zaidi ya Milioni 450 tumenunua magari 74 yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.7 na bajeyi zinaendelea kutengwa ili kuboresha suala la chanjo kuanzia ngazi ya taofa hadi chini” alisema Dk Leonard.


Dk: Dafrosa  Lyimo ni meneja  mpango wa taifa wa chanjo alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kutoka  mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza na Shinyanga ni  kuwahamasisha nakuwajengea uwezo waandishi hao ili kuendelea kutoa taarifa sahihi na  kuelimisha jamii kuhusu umhimu wa chanjo kwa watoto.


“Tunategemea baada ya kutoka hapa mtaendelea kuwa mabalozi wazuri ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti ili kuendelea kuibua mambao mbalimbali ili yaweze kuleta matokeo chanya katika jamii” alisema Dk Dafrosa.


             

Post a Comment

0 Comments