TANGAZA NASI

header ads

Wakulima wa viazi mviringo wachangamkia pembejeo za mkopo



Na Amiri Kilagalila,Njombe  

Wakati wakulima wakiwa katika maandalizi ya mashamba kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo cha zao la viazi mvilingo mkoani Njombe,wakulima wameanza kupokea pembejeo za kilimo kwa mkopo ili kuanza kilimo hicho mapema.

Wakulima walioanza kupokea pembejeo (Mbolea ) kwa ajili ya viazi ni pamoja na wanachi wa kijiji cha Iwungilo halmashauri ya mji wa Njombe,ambapo zaidi ya wakulima 200 wamepokea tani zaidi ya 24 kutoka shirika lisilo la kiserikali la One Acre Fund lililoanza kutoa pembejeo za mazao mbali mbali mwaka 2017 mkoani Njombe huku kwa zao la viazi ikiwa ni msimu wa pili.

Wakifafanua sababu ya kutoa mikopo ya mbolea kwa vikundi vya wakulima katika kijiji cha Iwungilo na maeneo mengine afisa mawasiliano ,Dorcas Tinga anasema wamelazimika kutoa mikopo ya pembejeo za kilimo kwa wakulima katika msimu huu wa kilimo ili kufanya kilimo cha kisasa na kwamba tani 770 zitatolewa katika mkoa wa Njombe huku tani 24 zikianza kutolewa kwa wakulima 200 wa kijiji cha Iwungilo.

“Kwanza mkulima ili akopesheke inatakiwa awe kwenye kikundi na kikundi kinatakiwa kuanzia watu 5 mpaka 16 na mkulima analetewa pembejeo hadi kijijini lakini mkopo huu inatakiwa alipe ndani ya mwaka mzima kuanzia siku anayopokea pembejeo hadi siku anapokuja kuvuna inatakiwa awe amelpa mkopo wake wote”alisema Dorcas Tinga

 Amesema anaamini wakulima watazitumia mbolea hizo kwa ajili ya kilimo cha viazi ili kupata mazao yenye tija kwa kuwa lengo lao ni kuhakikisha mkulima anakuwa na mbolea zote zinazotakiwa kwenye kilimo bila sababu ya kuosa fedha zitakazowasaidia kuendeleza kilimo.

Enihati Izrael ni msimamizi msaidizi kutoka shirika hilo wilaya ya Njombe,amesema wanaamini pembe jeo hizo zitawaongezea kipato wakulima huku kwa sasa baada ugawaji wa pembejeo zoezi litakalofuata ni mafunzo ya upanzi.

“Kitakachofuata tutaanza kutoa mafunzo ya upanzi wa viazi kwa wakulima maana yake tunavyotoa mafunzo wakulima wa huku kwa namna wanavyopanda viazi huwa wanapanda kabla ya mvua hazijaanza kunyesha kwa hiyo mvua zinapoanza kunyesha zinakuta viazi tayari vipo chini vimenza kuota”alisema Enihati Izrael

Elizabeth uhaula na Kaunti Danda ni baadhi ya wakulima waliofika kuchukua mbolea wanasema ukopeshaji wa mbolea umewasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wakati mwingine wamekuwa wakiishiwa fedha wakati msimu wa kilimo umekaribia.


“Kwa kweli wametusaidia sana kwasababu mwanzo tulikuwa tunapata shida unaweza ukawa ndani huna hela na msimu wa kilimo umefika lakini kupitia hili shirika unaweza ukachukua mbolea halafu ukawa unatoa hela kidogo kidogo,kwa kweli wametupa manufaa makubwa sanaa”alisema  Kaunti Danda

Nae mwenyekiti wa kijiji cha Iwungilo Mathayo Muyamba amesema kitendo kilichofanywa na shirika hilo kimedhamilia kuwainua wakulima na kutoa onyo kwa wakulima wanaolimbikiza madeni ya pembeo na kuacha doa kwa wengine.

Post a Comment

0 Comments