TANGAZA NASI

header ads

Serikali yatoa kauli usajili wa wachezaji 10 wa kigeni

 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu vilabu vya mpira wa miguu nchini kuendelea kusajili wachezaji 10 wa kigeni.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt.Harison Mwakymbe amesema hatua iliyochukuliwa na serikali ni baada ya kuzingatia maoni ya wadau.

Pia amesema bado wizara kwakushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kitako kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa nankuingia Nchini.

"Angalau nchi zilizopo katika nafasi ya 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata wa daraja la kwanza,ingawa bado hii si sheria ni maoni tu" Alisema Mwakyembe.

"Ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka Nje wawe na weledi,wawe na uwezo mkubwa"

Amesema kati watu 977 waliyotoa maoni ,watu 809 wametaka idadi ya wachezaji 10 wakigeni

Kando na hayo Wizara imeagiza watu wanaoajiriwa Nchini wawe na ulazima wa kujifunza/kufunzwa Kiswahili.

Hata hivyo kutakuwa na majadiliano juu ya viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajili nchini.

Post a Comment

0 Comments