TANGAZA NASI

header ads

NEC yawaidhinisha Magufuli na Mama Samia kugombea

 

Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage kwa mamlaka aliyopewa amemteua Dkt Magufuli kuwa mgombea wa Kiti cha Urais na Mama Samia kuwa mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais kupitia CCM na kukabidhiwa seti za fomu na nyaraka muhimu kuwa kumbukumbu kwao.

Hayo yamejiri leo Agosti 25, 2020, katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Jijini Dodoma mara tu baada ya Rais Magufuli na mgombea mwenzake kurudisha fomu za uteuzi kutoka NEC na kuonekana kuwa wanazo sifa za kugombea kupitia CCM.

Katika safari yake ya kutafuta wadhamini, Rais Magufuli amepata wadhamini kutoka Mikoa 20, na wamewasilisha stakabadhi ya malipo ya kiasi cha Shilingi Milioni 1 na wote wameapa kwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Zoezi la urejeshaji wa fomu za uteuzi kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), litahitimishwa leo Agosti 25, 2020, majira ya saa 10:00 jioni

Post a Comment

0 Comments