TANGAZA NASI

header ads

Barcelona yapanga kujenga timu nyuma ya Messi



 Messi anashikilia nafasi ya kwanza ya Barca ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa kutikisa wavu mara 634Image caption: Messi anashikilia nafasi ya kwanza ya Barca ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa kutikisa wavu mara 634

Barcelona bado inapanga kujenga timu kwa kumtumia Lionel Messi na wanajaribu kumshawishi aendelee kubakia katika klabu hiyo, anasema Mkurugenzi wa mchezo Ramon Planes.

Messi mwenye umri wa miaka 33-anayecheza katika safu ya mashambulizi kutoka Argentina aliiambia klabu hiyo kuwa anataka kutekeleza kipengele cha mkataba wake kinachomruhusu kuondoka bila malipo.

Mshindi huyo wa mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or ndiye anayeshikilia nafasi ya kwanza ya Barca ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa kutikisa wavu mara 634.

"Kile kilichotokea kimetokea na wazo letu ni kuijenga timu kwa kumtumia mchezaji muhimu duniani ," anasema Planes.

"Tunataka kujenga msururu mwingine wa ushindi ukiongozwa na mchezaji bora duniani, bora katika historia.

"Barca na Leo ni kama ndoa, kwani wote wamejitolea sana miongoni mwao, na wameleta furaha sana kwa mashabiki. Ninadhani hali ya baadae ni nzuri. Nina matumaini."

Messi - anataka kuondoka Barcelona baada ya timu hiyo kushindwa kupata kombe katika msimu uliomalizika kwa kuchapwa 8-2 na Bayern Munich katika michuano ya robo fainali ya kuwania kombe la Ulaya.

Post a Comment

0 Comments