TANGAZA NASI

header ads

Wanajeshi wa Rwanda na Burundi wakutana kujadili mzozo baina ya nchi zao

 


Wanajeshi wa Burundi (katikati)wakizungumza na manajeshi wa Rwanda (kushoto) pamoja na mwakilishi wa ICGLR (kushoto) katika mpaka wa NembaImage caption: Wanajeshi wa Burundi (katikati)wakizungumza na manajeshi wa Rwanda (kushoto) pamoja na mwakilishi wa ICGLR (kushoto) katika mpaka wa Nemba

Katibu wa Jumuiya ya nchi za maziwa (ICGLR) amesema kuwa mkutano wa kwanza unaowashirikisha wakuu wa upelelezi wa majeshiya Rwanda na Burundi ni mwanzo mzuri na fursa kubwa ya mataifa hayo kutatua mzozo baina yao.

Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Kanali Ernest Musaba na ule wa Rwanda ukiongozwa na Brigadia Jenerali Vincent Nyakarundi wamekutana kwenye mpaka wa nchi hizo mbili katika kikao kinachoongozwa na muwakilishi kutoka ICGLR Leon Mahoungou.

Katibu Mkuu wa ICGLR Zakary Muburi-Muita ameiambia BBC kuwa mkutano huo unalenga kuwezesha nchi hizo kurejesha uhusiano mwema wa kijeshi na baadae kisiasa.

"Mnafahamu kuwa nchi hizi mbili zimekuwa na uhusiano mbaya wa kisiasa na kijeshi kwa muda mrefu " Mubur Muita, aliiambia BBC.

Uhusiano baina ya nchi hizi mbili umekua mbaya tangu mwaka 2015, na mwezi mei kulikuwa na na mapigano baina ya majeshi ya pande mbili karibu na mpaka wa nchi mbili eneo la ziwa Rweru.

Kila upande umekuwa ukiulaumu mwingine kuwaunga mkono waasi wa mwenzake na kuyumbisha usalama.

Post a Comment

0 Comments