Waziri wa Madini, Dotto Biteko ameipongeza Kampuni ya Uchimbaji
wa Madini ya dhahabu - Geita (GGML) kwa kuwa mfano katika kuchangia
utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo katika ziara fupi aliyoifanya mkoani
Geita na kukagua miradi inayotekelezwa na Kampuni ya GGML chini ya mpango wake
wa kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility) katika Mji wa Geita.
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuona maisha ya watu katika
maeneo yote yenye rasilimali ya madini, ikiwemo Geita yanabadilika kiuchumi na
kwamba anafurahishwa na namna ambavyo Serikali ya Mkoa wa Geita inavyosimamia
ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye sekta ya madini.
"nukuu"
"Tayari tumeshafikia lengo la kukusanya zaidi ya Sh bilioni
400 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 kutoka kwenye sekta hii, na sehemu
kubwa ya makusanyo haya imetoka Geita, hususan GGML. Inatia moyo sana kuona sekta
hii sasa inachangia zaidi ya asilimia 5 ya uchumi wa nchi yetu. Lengo ni
kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025,"amesema
Waziri Biteko.
Moja ya miradi ambayo ilikaguliwa na Biteko katika ziara
yake ni ujenzi wa Kanda maalumu ya uwekezaji "Special Economic
Investment Zone" ambao utasimamiwa na Mamlaka ya ukanda maalumu wa
Uwekezaji (EPZA) na Halmashauri ya Mji wa Geita.Pia ametembelea miradi mingine
ya kimkakati inayofadhiliwa na GGML, ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu la Geita Mjini
na soko la Katundu.
0 Comments