Kamishna
Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa, Swagile Msananga amewatoa hofu
wananchi wa Mkoa huo kuwa, hawatakuwa na haja ya kusafiri umbali
mrefu
kufuata huduma za sekta ya ardhi katika ofisi za kanda zilizopo mkoa wa
Mbeya baada ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini,
kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa zikiwa na lengo la kusogeza huduma
hizo karibu na wananchi
Msananga amesema kuwa lengo la wizara
kuwapunguzia wananchi gharama za usafiri kufuata huduma ambazo hivi sasa
zinapatika katika ofisi hizo zilizopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa
mkoa wa Rukwa, huku akifafanua huduma zinazotolewa kuwa ni pamoja na
masuala ya mipango miji, uthamini, upimaji na ramani, usajili wa hati na
kusaini hati.
“Sasa Wananchi badala ya kufunga safari kwenda
mbeya kupata huduma, hizo safari sasa hazitakuwepo tena, huduma zote
zitapatikana hapahapa, na halmashauri zote ambazo tunazihudumia pia
zitaleta nyaraka zao hapa kwaajili ya kupata idhini na hati zitasainiwa
hapahapa, na nyaraka zote zitasajiliwa hapa.”
“Kwahiyo napenda
niwape wananchi taarifa kwamba ofisi ya Kamisha wa Ardhi Mkoa wa Rukwa
imeshaanza kazi rasmi na tunawakaribisha mpate huduma zote na tunaahidi
kwamba tutawapa huduma katika ubora na uadilifu,” Alisema. Hivi karibuni
tarehe 10, Mei 2020 akiwa jijini Dodoma Waziri wa Ardhi Maendeleo ya
Makazi Mh. William Lukuvi alisema Wizara hiyo imeanzisha ofisi za ardhi
katika kila Mkoa ili kutoa huduma zote zilizokuwa zinatolewa kwenye
ofisi za Kanda na Makao Makuu.
0 Comments