Na Henrick Idawa,Makete
Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani
Njombe imepongezwa kwa kupata hati safi 2018/2019 na kupunguza hoja za mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa serikali CAG kutoka 44 zilizokuwepo na kubaki 24
Hayo yamebainika leo katika Baraza
maalum la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Makete lililokuwa na lengo la
kujadili hoja za Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa serikali ambapo Katibu Tawala Mkoa
wa Njombe Katarina Revocati ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Njombe
ameonesha kufurahishwa na jambo hilo
Mbali na pongezi hizo pia ameitaka
halmashauri hiyo kuhakikisha inasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na
ihakikishe wakusanyaji wanafikisha mapato hayo ya serikali benki kama sheria
inavyotaka ili kuepuka upotevu wa mapato
Naye Mkuu wa wilaya ya Makete Mh
Veronica Kessy amekemea vitendo vya baadhi ya watendaji kufuja mapato ya
serikali kwa kutumia fedha hizo kwa matumizi yao binafsi kinyume cha sheria
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Makete Mh Egnatio Mtawa amemtoa shaka katibu Tawala wa Mkoa kwamba tayari
wameweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha mapato yakikusanywa yanafikishwa benki.
Diwani wa kata ya Mlondwe Mh. Alphonce
Salim amesema upatikanaji wa hati safi kwa halmashauri ni jambo jema walilokuwa
wakilitaka muda mtefu

0 Comments