Na Jackline Kuwanda,DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli amesema kuwa ufaulu katika shule za msingi na Sekondari
umeongezeka.
Ufaulu wa Darasa la Nne umefikia asilimia 91.9%,
Darasa la saba ukiongezeka kutoka 57 % mwaka 2015 hadi 81.5 % mwaka 2019 huku
ufauli wa kidato cha nne ukiongezeka kutoka 69.8% mwaka 2015 hadi kufikia
80.65% mwaka 2019.
Rais Magufuli ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati
akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT),ambapo amewapongeza
walimu kote nchini kwa kuwezesha kupatikana kwa mafaniko hayo kwani bila ya
walimu kutoa ushirikiano huo mafaniko hayo yasingepatikana huku akisema kuwa
ataendelea kuwalipa walimu mishahara yao licha ya kuwa shule zimefungwa
kutokana na janga la corona.
Amesema walimu ndio wazalishaji wa sekta zote
hivyo hawana budi kutambua ,kuenzi na kuthamini mchango wa walimu katika
nchi huku akibainisha kuwa licha ya uwepo wa mafaniko katika sekta ya
elimu lakini anatumbua kuwa zipo changamoto katika sekta hiyo ambazo
zimeendelea kuwepo kwani serikali inazifahamu na inaendelea kuzishghulikia
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa
baada ya kufanyika kwa zoezi la uhakiki serikali tayari imewapandisha vyeo
watumishi laki tatu na sita na mia tisa kumi na saba ambapo walimu wakiwa ni
laki moja sitini elfu na mia tatu sitini na saba
Awali akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi Katibu
Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Comred Mwalimu Deus Seif amesema kuwa
chama kinatambua jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha maisha ya
watanzania ikiwemo walimu kwani kwa upande wa sekta ya elimu yapo
mambo mbalimbali ambayo serikali imeyafanya kwa kipindi cha miaka mitano
ikiwemo ongezeko la miundombinu na samani,upandishaji wa madaraja na
marekebisho ya mishahara kwa walimu huku akibainisha changamoto zilizopo licha
ya mafaniko yaliyopo.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wote Nchini Tanzania
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya amempongeza Rais Magufuli
kwa kuendelea kuenzi tasinia ya ualimu kwani amehakikisha kuwa mahitaji yote
muhimu walimu yanapatikana.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Bunge,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mh Jenista Mhagama amelipongeza shirikisho
la vyama vya wafanyakazi na viongozi wake hapa nchini kwa kuwa viongozi imara
kwani wameweza kuongeza vyema vyama hivyo.


0 Comments